Na Mwandishi Wetu, Arusha
MKURUGENZI wa Jiji la Arusha Bw Athuman Kihamia amekataa kamati ya watu 4 mbele ya Baraza la madiwani wa Jiji la Arusha iliyokuwa imepangwa kwa ajili ya kuchunguza mgogoro wa maduka hayo 396 yalipo stand ndogo Jiji la Arusha kwa kile alichosema kuwa wananchi bado wanawatuhumu madiwani wengi kuwa chanza cha migogoro hiyo.
Mkurugenzi huyo amesema kuwa binafsi haoni sababu za msingi za uwepo wa kamati hiyo badala yake ana hofu ya kuingizwa siasa katika jambo hilo.
Kuhusu wajenzi wa vibanda vya maduka stand ndogo, Mkurugenzi wa jiji la Arusha Bw Athumani Kihamia amewataka madiwani kutokuweka maneno ya kisiasa katika swala hilo la kimaendeleo ambapo mpaka sasa mgogoro wa maduka hayo takribani 396 upo katika mahakama ya ardhi jiji la Arusha.
Aidha pia mkurugenzi wa jiji la Arusha ameongeza kwa kusema kuwa mapato makubwa ya jiji la Arusha yalikuwa yanakusanywa kupitia maduka hayo takribani 1196 hapa jijini maduka hayo ambayo yapo maene ya Stand ndogo, Soko kuu, Kilombero na kijenge ambapo halmashauri ilikuwa inakusanya shilingi Bilioni 1.2 kwa mwaka kitu ambacho kwasasa ameeleza kuwa mapato hayo yanaweeza kupungua kutoka na mgogoro wa maduka 396 yalipo maeneo ya Stand ndogo jijini Arusha na kubaki maduka 800 yanayo tegemewa na halmashauri hiyo ya jiji la Arusha
Diwani wa kata ya Olasiti Bw Alex Mart ameeleza kuwa katika utatuzi wa migogoro ya wananchi inahitajika umoja na ushirikiano wa viongozi wote kuwa kitu kimoja pasipo kujali itikadi ya vyama vyao pamoja na nyazifa walizo nazo badala yake busara itumike katika utatuzi wa migogoro hiyo.