Mgogoro wa Kugombea Ziwa Nyasa Kati ya Tanzania na Malawi Wapelekwa SADC

Ziwa Nyasa

MGOGORO wa kugombea nani ni mmiliki wa Ziwa Nyasa kati ya nchi za Tanzania na Malawi umezidi kuwa mgumu baada ya kushindwa kuafikiana tena leo kati ya kikao cha mawaziri wa nchi hizo mbili pamoja na wanasheria wao.
Kutokufikia mwafaka huku kumejitokeza leo baada ya kikao hicho hivyo pande zote kukubaliana suala hilo liende kuamuliwa na jopo la marais wastaafu wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC). Hata hivyo Tanzania imesema endapo SADC watashindwa kutatua suala hilo litapelekwa tena katika Mahakama ya Usuluishi wa Migogoro Kimataifa ili haki ipatikane.

Mvutano huo umeibuka zaidi pale nchi ya Malawi ilipoanza kuingiza makampuni ya utafiti wa mafuta na gesi ambayo yaliingia na kuweka kambi hadi maeneo ya Tanzania. Tanzania imekuwa ikiamini ziwa hilo ni miliki ya nchi hizi mbili, huku Malawi ikipinga na kutaka itwae ziwa lote.