Mganda Awasili Dar Kumkabili Bondia Mashali, Wapima Uzito

Bondia THOMAS MASHALI kushoto akitunishiana misuri na MEDY SEBYALA wa UGANDA baada ya kupima uzito Dar es salaam leo kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika siku ya kumbukumbu ya baba wa Taifa katika pambano la Ubingwa wa Africa mashariki litakalofanyi ukumbi wa Friends corner Hotel Oktoba 14, 2012a katika anaeshudia katikati ni Rais wa TPBC Onesmo Ngowi ambaye ndie msimamizi mkuu wa mpambano huo. Picha na Super d blog

BINGWA wa Uganda Medy Sebyala amewasili nchini Tanzania kwa ajili ya pambano lake la ngumi na Bingwa wa Taifa wa Tanzania, Thomas Mashali, katika pambano la Ubingwa wa Africa Mashariki na Kati litakalo fanyika kwenye Ukumbi wa Friends Corner Hotel Oktoba 14, 2012.

Akizungumzia pambano hilo Katibu Mkuu Msaidizi, Said Chaku ambaye alikuwa pamoja na Rais wa TPBO, Yasin abdallah wakati wa mapokezi ya bondia huyo aliefuatana na mwalimu wake tokea Uganda, ni kuwa wamefika salama na wapo katika hali nzuri ya ushindani na muda wote mganda huyo, Med Sebyala alionekana mwenye kujiamini na kujitapa kwamba amekuja kumuangamiza mpinzani wake (Mashali) na kuondoka na mkanda wa ubingwa kwao.

Pambano hilo la ubingwa wa Afrika Mashariki litasimamiwa na Organization ya Ngumi za kulipwa nchini-TPBO, chini ya Yasin Abdallah na mabondia hao watapima uzito na afya kiujumla Oktoba 13, 2012 saa tatu asubuhi Friends Corner Hotel. Shughuli zima la upimaji litasimamiwa na katibu mkuu wa TPBO bw Ibrahim Kamwe na dr Donald Madono pia kutakuwepo na mapambano zaidi ya sita ya utangulizi.

Wakati huo huo; Mpambano wa kugombea mkanda wa Shirikisho la Ngumi la Afrika ya Mashariki na Kati (ECAPBA) katika uzito wa kati (Middleweight) kati ya bondia Thomas Mashali na Sebyala Med wa Uganda umechukua sura mpya baada ya mabondia wote kutambiana wakati wakipima uzito leo katika ukumbi wa Friends Corner, Manzese jijini Dar-es-Salaam.

Rais wa Shirikisho la Ngumi za Kulipwa la Afrika ya Mashariki na Kati (ECAPBA) Onesmo Ngowi alisimamia shughuli ya kuwapima uzito wakali hao. Ngowi ambaye pia ni Rais wa IBF katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati, Ghuba ya Uarabu na Ghuba ya Uajemi, Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Nchini (TPBC) na Mkurugenzi wa Baraza la Ngumi la Jumuiya ya Madola (CBC) alisema kuwa ECAPBA iko tayari kusimamia pambano hilo linalofanyika kesho siku ya Nyerere Day Octoba 14 jumapili katika ukumbi wa Friends Corner, Manzese.

Promota wa mpambano huo uliopewa jina la “Vurumai ya Manzese” (Rumble in Manzese)” ni Selemani Semunyu ambaye anajulikana kwa kutoa vipindi muruwa vya Televisheni ya ITV. Mshindi katika pambano hili atakuwa ndiye mbabe wa uzito wa kati (Middle) katika nchi 11 za Afrika ya Mashariki na Kati.

Wasimamizi wa mpambano huo ni: Onesmo Ngowi: Msimamizi Mkuu (Supervisor)

Nemes Kavishe: Refarii

Mark Hatia: Jaji namba 1

Said Chaku: Jaji namba 2

Sakwe Mtulya: Jaji namba 3

Imetolewa na: Utawala Shirikisho la Ngumi za Kulipwa la Afrika ya mashariki na Kati (ECAPBA)