Waandishi wa Habari wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Emmanuel Humba wakati wa mkutano kati yao uliofanyika leo jijini Dar es Salaam kuhusu mfuko huo kutimiza miaka kumi tangu kuanzishwa kwake mwaka 2001 ambapo waziri Mkuu Mizengo Pinda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo zitakazofanyika tarehe 19 mwezi huu.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Emmanuel Humba (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mfuko huo kutimiza miaka kumi tangu kuanzishwa kwake Machi 19 ambapo Waziri Mkuu Mizengo Pinda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe zitakazofanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Fedha, Mipango na Uwekezaji Deusdedit Rutazah akifuatiwa na Eugen Mikongoti ambaye ni Mkurugenzi Mwezeshaji wa Mfuko huo.
Mkurugenzi Mwezeshaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Eugen Mikongoti akijibu maswali ya waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mfuko huo kutimiza miaka kumi tangu kuanzishwa kwake mwaka 2001 ambapo waziri Mkuu Mizengo Pinda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe zitakazofanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu Emmanuel Humba na kulia ni Mkurugenzi wa Fedha, Mipango na uwekezaji Deusdedit Rutazah. Picha zote na Anna Nkinda - Maelezo