Mfanyakazi UN Aliyeambukizwa Ebola Afariki

Mgonjwa wa Ebola

Mgonjwa wa Ebola

MFANYAKAZI wa Umoja wa Mataifa aliyeambukizwa Ebola amefariki dunia katika hospitali moja nchini Ujerumani. Madaktari katika hospitali ya Leipzig wamesema mtu huyo mwenye umri wa miaka 56, alifariki dunia mapema Jumanne asubuhi.

Mlipuko huo umeua zaidi ya watu 4,000 tangu mwezi Marchi, mwaka huu hususan katika nchi za Liberia, Sierra Leone, Guinea na Nigeria. Shirika la Afya Duniani limeuelezea ugonjwa huo kama tatizo la dharura la kiafya kuwahi kuonekana katika maisha ya sasa ya binadamu.

Marekani na Uingereza ni miongoni mwa nchi zilizoanzisha utaratibu wa upimaji afya za abiria kuhusiana na ugonjwa wa Ebola katika viwanja vya ndege.
-BBC