Meya wa Jiji la Dar Amtembelea Mjane wa Bob Makani

Mjane wa aliyekuwa mhasisi na Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kaboga Makani akizungumza jambo na Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita mara baada ya kumtembelea Nyumbani kwake mapema leo asubuhi.

 

Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akimfariji Mjane wa aliyekuwa mhasisi na Katibu MKuu wa kwanza wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Bob Makani (Mama Makani).

 

Na Christina Mwagala, OMJ

MEYA wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita leo amemtembele mjane wa aliyekuwa Mhasisi na Katibu Mkuu wa kwanza wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Bob Makani , Mama Kaboga Makani ikiwa ni moja ya ziara zake za kutembelea wazee pamoja na viongozi ambao waliwahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya jiji la Dar es Salaam.

Meya ambaye amerejea Nchini jana kutoka Nchini Iran ambapo alikuwa kwa ziara ya kikazi ya siku 10, amesema kwamba hatua ya kutembelea viongozi pamoja na wazee ambao ni waasisi inalenga kutambua michango yao katika nafasi ambazo waliwahi kutumikia na kwamba busara zao pia ndio zimeweza kulifikia Taifa sehemu ilipo hivi sasa.

Alifafanua kuwa Bob Makani enzi za uhai wake alikuwa ni mmoja na mwa sisi wa Chadema na kwamba anatambua mchango wake kutokana na juhudi alizozionyesha ikiwemo kukipigania chama hadi kufikia kilipo hivi sasa.

Alisema Bob Makani pamoja na wenzake ndio waliokianzisha Chama Cha Chadema na kufika mbali zaidi kwamba bila wao hata yeye asingekuwa Meya wajiji hili kupitia chama hicho na kwamba mchango wao ndani ya chama bado utaendelea kukumbukwa na kila mmoja wakiwemo wanachama wa chama hicho na wananchi kwa ujumla.

Alisema Bob Makani mbali na kuwa mwanachama na mwasisi wa Chadema lakini pia aliwahi kuwa Gavana wa Benki kuu ambapo alitumikia nafasi hiyo kwa na hivyo baada ya kustaafu nafasi hiyo aliamua kuanzisha chama na hivyo kuwepo hadi hivi sasa.

“Haya sio mambo ya kisaisa , lakini unaweza kuona kwamba ni alikuwa mtu muhimu, lakini pia kama kijana wao lazima nipate basara kutoka kwao, ingawaje hatunaye tena hapa duniani, lakini huko alipo anaona jambo gani ambalo tunafanya kama vijana ambao alituacha ndani ya chama,” alisema.

Alifafanua kwamba jambo la kutembelea viongozi ama waasisi wa nafasi chama sio jambo la kisiasa bali ni kutokana na kutambua mchango wakazi ambazo waliwahi kuzifanya wakati huo.

“Ziara hii sio ya kwa Mzee Makani tu, ila ni kwa waasisi, na wale ambao waliwahi kuwa viongozi wa jiji, wapo nitawatembelea, ikiwa ni sehemu yangu pia ya kutambua mchango wao, sambamba na kupata baraka, busara zao ambazo walizitumia katika uongozi wao, ukizungumza vizuri na wazee hawa unapata baraka na kuona kwamba namna gani unaweza kuwaongoza wananchi,” alisema Meya Mwita.

“ Nimekuja leo kumuona Mama yetu, naweza kusema ni mama yetu kwa sababu kila mmoja anamfahamu mzee Makani, alikipigania chama, na ndio katibu mkuu wa wa kwanza ndani ya Chadema, kama vijana hatuna sababu ya kuwasahau wasisi wetu, wazee wetu, watu ambao tunawatambua kabisa waliitumikia nchi yetu,” alisema Meya Isaya.