Meya Kinondoni Awakabidhi Soko Wafanyabiashara Ndogondogo

Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusufu Mwenda (katikati) na viongozi wengine wakitembelea vizimba vya soko jipya la SIMU 2000

Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusufu Mwenda (katikati) na viongozi wengine wakitembelea vizimba vya soko jipya la SIMU 2000

Na Mwandishi Wetu
MSTAHIKI Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusufu Mwenda amesema kuwa soko jipya la SIMU 2000 litaweza kuchukua wafanyabiashara 512 kutoka kila pembe ya Manispaa ya Kinondoni.

Mwenda amewatoa hofu wafanyabiashara wa soko jipya la kituo cha basi cha Simu 2000 mawasiliano kuwa watafanya biashara bila ya kuwa na matatizo yoyote kwa kuwa soko hilo lipo katika mfumo wa kisasa.

Mwenda alisema hayo alipokuwa akikabidhi vizimba vya soko hilo kwa wafanyabiashara ndondogo waishio katika Wilaya ya Kinondoni na sio mtu kutoka eneo la nje ya manispaa hiyo hivyo kuwataka kulitunza soko hilo kama mali yao.

“Tumeamua kulifanya soko hili hili liweze kuanza kazi kabla ya uzinduzi rasmi utakaofanywa baadae hili kuweza kuwapa fursa wafanya biashara kuliko kuacha jingo limeisha na kuonekana kama picha hivyo nawaomba mfanye biashara hili muweze kujiongeza kipato,” alisema Mwenda.

Alitoa wito kwa wafanyabiashara hao kutokata tama kwani mwanzo ni mgumu kwnai eneo lenyewe ni jipya hivyo sio rahisi kuona biashara ikichanganya kwa haraka kama wanavyofikiri.