Baadhi ya vitu na vyakula ambavyo vilikabidhiwa kwa kikundi cha kulea wasichana waliokuwa wanaishi katika mazingira magumu New Hope For Girls Organization ambapo mama Consoler Eliya analea wasichana 147 . Hafla hiyo ilifanyika katika makazi ya waziri mkuu 07/02/2014 jijini Dar es salaam .
Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda akimkabidhi msaada wa vyakula nguo na vitu vigine vyenye thamani ya shilingi million 6.8/- ambavyo ni michango kutoka kwa kikundi cha wake wa viongonzi (Mellinium Women Group ) kwa mama Consoler Eliya wa kituo cha New Hope for Girls Organization cha Tabata jijini DSM analea wasichana ambao walikuwa wanaishi katika mazingira magumi.wa kwanza kulia ni Prisca Vicent mmoja kati ya wasichana 147 wanaolelewa na kituo hicho na hafla hiyo ilifanyika ijumaa 07/02/2014 katka makazi ya waziri mkuu jijini Dar es salaam .
Mwenyekiti wa kikundi cha Wake wa Viongonzi (Mellinium Women Group) Mama Lukuvi akimkabidhi Consoler Eliya (mwenye miwani ) kutoka New hope for Girls Organization ya Tabata jijini Dar es salaam ambaye analea wasichana 147 waliokuwa wanaishi katika mazingira magumu . Jumla ya msaada huu ni shikingi milioni 6.8/-ambayao ni michango kutoka kwa wake wa viongonzi . Hafla hiyo ilifanykia katika makazi ya waziri mkuu jijini Dar es salaam ijumaa 07/02/2014. Na wakwanza kulia ni msichana Halima Seleman na Paschallia Kaimbe. Picha zote naOfisi ya Waziri Mkuu