Mechi za VPL wikiendi hii

Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura

WIKIENDI hii kutakuwa na mechi nne za VPL. Mechi za Jumapili (Februari 19 mwaka huu) ni kati ya Coastal Union itakayoikaribisha Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga wakati Villa Squad itakuwa mgeni wa Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro. Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Polisi Dodoma.

Wakato huo huo, mechi za Ligi Daraja la Kwanza (FDL) zinaendelea wikiendi hii ambapo kesho, Februari 18 mwaka huu kutakuwa na mechi ya Kundi C kati ya Polisi Morogoro na Rhino FC ya Tabora itakayochezwa Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Februari 19 mwaka huu Kundi A ni kati ya Morani FC na Temeke United zitacheza mkoani Manyara na Februari 20 mwaka huu ni Transit Camp na Polisi Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Burkina Faso na Mgambo Shooting kwenye Uwanja wa Jamhuri.

Kundi B Februari 19 mwaka huu Small Kids itaikaribisha Mbeya City kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, Mlale na Polisi Iringa kwenye Uwanja wa Majimaji na Tanzania Prisons na Majimaji kwenye Uwanja wa Sokoine.