Mechi ya Uingereza na Italia Yaongoza kwa Idadi ya Pasi

Mchezo kati ya Italia na Uingereza ukichezwa.

Mchezo kati ya Italia na Uingereza ukichezwa.

Mchezaji Thomas Mueller (24) wa timu ya taifa ya Ujerumani akipiga mpira golini.

Mchezaji Thomas Mueller (24) wa timu ya taifa ya Ujerumani akipiga mpira golini.

MECHI ya mchezo wa fainali za Kombe la Dunia kundi ‘D’ kati ya timu ya Taifa ya Uingereza na Itali ndiyo inayoongoza kwa kuwa mechi pekee ambayo ilikuwa na idadi kubwa ya pasi kuliko mechi zote zilizochezwa hadi Juni 20, 2014 kwa mujibu wa takwimu za FIFA.

Mechi hiyo ambayo timu ya Taifa ya Italia waliwabugiza Uingereza kwa mabao 2 kwa 1223, huku wachezaji wa timu ya Italia wakiongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya pasi walizopika katika mchezo huo uliokuwa na kasi ya kuvutia. Italia walipiga jumla ya pasi 606 huku wenzao wa Uingereza wakiwa wamepiga pasi 467 hadi kipenga cha mwisho kinapulizwa.

Kinara wa upigaji pasi katika mchezo huo alikuwa ni mchezaji wa timu ya taifa ya Italia, Daniele De Rossi ambaye alipiga jumla ya pasi 101. Kwa mujibu wa FIFA mechi inayofuatia kwa kuwa na idadi kubwa ya pasi hadi sasa ni ile ya Chile na Australia ya kundi ‘B’ ambapo ilikuwa na jumla ya pasi 1164, huku Chile ikiongoza kwa kupiga jumla ya pasi 729.

Kwa upande wa wapinzani wao timu ya Australia walipiga jumla ya pasi 435, lakini hadi mchezo huo unamalizika Chile waliibuka mshindi baada ya kumchapa mpinzani wake 2-1. Nafasi ya tatu ya mechi iliyokuwa na pasi nyingi imechukuliwa na Mechi kati ya Spain na Chile ambapo ilikuwa na pasi 1169.

Katika mchezo huo Spain ndio waliokuwa na idadi kubwa ya pasi yaani 705 na wapinzani wao pasi 464 Kwa upande wa magoli timu ya taifa ya Uholanzi ndiyo yenye idadi kubwa ya magoli ambapo ina magoli nane ya kufunga, huku ikifuatiwa na timu ya taifa la Ufaransa yenye magoli 7 hadi sasa.

Timu za Chile na Colombia kwa pamoja ndio zinazoshika nafasi ya tatu kwa kuwa na magoli 5 kila moja. Mchezaji anayeongoza kwa kufuga magoli hadi jana alikuwa ni Thomas Mueller (24), mwenye magoli matatu