Mechi ya Kagera Sugar Vs Coastal yasogezwa mbele

Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura.

MECHI namba 89 ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Kagera Sugar na Coastal Union iliyopangwa kufanyika Novemba 2 mwaka Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba imesogezwa mbele kwa siku moja.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) kupitia Ofisa Habari wake, Boniface Wambura imesema uamuzi wa kusogeza mechi hiyo hadi Novemba 3 mwaka huu umetokana na wamiliki wa Uwanja wa Kaitaba kuruhusu utumike kwa sherehe za Mwenge wa Uhuru.