Mchezaji wa Soka Marekani Ajitangaza Shoga

Mchezaji, Michael Sam

Mchezaji, Michael Sam

MCHEZAJI mmoja wa timu ya mpira wa miguu ya nchini Marekani, National Footbal League (NFL), Michael Sam amejitangaza kuwa yeye ni shoga. Sam anakuwa ni mchezaji wa kwanza kutangaza wazi kwamba yeye ni shoga katika mchezo wa mpira wa miguu Marekani.

Sam alikuwa ameteuliwa na timu ya Saint Louis Rams katika siku ya mwisho ya usakaji wa vipaji katika mchezo huo ulio maarufu zaidi nchini marekani. Hatua hiyo ya Michael Sam kutangaza jinsia yake mnamo mwezi Februari baada ya kukamilisha masomo yake ya mchezo huo katika Chuo cha Missouri ilipongezwa na watu mbalimbali akiwemo, Rais wa nchi hiyo Barack Obama.

Hata hivyo baadhi ya wachambuzi wa michezo nchini Marekani wamebashiri huenda kitendo hicho kikamuathiri mchezaji huyo kwa kile baadhi ya timu kuhofia umaarufu wa mchezaji huyo kwa sasa na kutokana na hatua aliyofikia sasa.
-BBC