Mchekeshaji Bill Cosby Atiwa Hatiani Kwa Dhuluma ya Kimapenzi

http _hss-prod.hss.aol.com_hss_storage_midas_73fc931c72c0f020f713fad5f7469f90_202244964_243439081
Waendesha mashtaka katika jimbo la Pennsylvania Nchini Marekani wamemfungulia mashtaka ya kwanza mchekeshaji nguli Bill Cosby .

Cosby ameshtakiwa kwa makosa ya dhuluma za kimapenzi dhidi ya mfanyikazi mmoja wa chuo kikuu kimoja nchini Marekani,Kosa hilo lilifanyika mwaka wa 2004.
Awali mchekeshaji huyo alikana kuwadhulumu kimapenzi akijitetea kuwa aliwahi kushiriki mapenzi baada ya kukubaliana na wanawake hao.
141208121102-bill-cosby-exlarge-169
Mashtaka dhidi yake yalifufuliwa baada ya idadi kubwa ya wanawake kuibuka wakidai walipewa dawa na kisha kudhulumiwa kimapenzi na mchekeshaji huyo nguli.
Bi Andrea Constand, aliyekuwa mfanyikazi wa chuo kikuu cha Temple ndiye aliyemshtaki Cosby mara ya kwanza mwaka wa 2005

Uchunguzi ulibaini kuwa bwana Cosby alikuwa akiwapa wahasiriwa dawa aina ya Quaaludesinawalegeza na hat wengine wanasinzia kabla ya kushiriki mapenzi nao huku Cosby akikiri kutumia dawa hizo za Quaaludes.