ZIKIWA zimepita siku mbili toka uongozi wa Serikali ya Tarafa ya Mawengi Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe kuwapongeza wadau mbalimbali waliojitokeza kuchagia Shule ya Msingi Ludewa
mjini iliyokubwa na maafa ya kimbunga na madarasa matatu kuezuliwa na uongozi wa tarafa hiyo kuwashukuru waliojitokeza kuchangia akiwemo Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Pindi Chana (Mb) kiasi cha Tsh 15,000 huku waziri huyo akikanusha kuchangia ukweli zaidi wa mchango wa waziri umewekwa hadharani. Ifahamike wazi kuwa shule hiyo ilikumbwa na maafa ya
kuezuliwa kwa paa zake za vyumba hivyo vitatu na hivyo kupelekea watoto zaidi ya 200 kukosa sehemu ya kusomea na hivyo kulazimika kubanana katika vyumba vilivyopo toka Februari 28 mwaka huu maafa hayo yalipojitokeza. Si mzazi wala mwalimu au serikali ngazi ya kijiji hadi Taifa ambayo ilipenda kutokea kwa maafa hayo kwani hilo lilikuwa ni pigo kubwa kwa shule hiyo na njia pekee ya kutatua ilikuwa ni serikali kupitia kitengo cha maafa, Halmashauri ama wadau mbalimbali wakiwemo wananchi na viongozi wao kama madiwani na wabunge kwa maana ya mbunge wa jimbo na mbunge wa viti maalum.
Katika kuliona hilo Waziri Pindi ambae ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Njombe kupitia (CCM) alifika shuleni hapo Mei 5, 2014 na kuwapa pole walimu kwa maafa hayo na zawadi nyingine alizotoa vitu vya kujisomea wanafunzi na kalamu moja moja kwa walimu wote jambo lililofanya walimu kukumbuka zaidi alitoka kalamu
zenye nembo ya CCM na zenye jina lake, Pindi Chana jambo ambalo si baya na linapaswa kuungwa mkono kwa kila mdau wa maendeleo ya elimu katika kuwapa motisha walimu wetu. Waziri Chana ambae ndie wizara yake inahusika na watoto kwa kuliona tatizo hilo la vyumba vya madarasa kuezuliwa alionesha kuguswa zaidi na hata kuwa kiongozi wa kwanza kuanza kuchangia mchango kwa ajili ya harambee ya ujenzi wa vyumba hivyo kwa kuchangia shs 15,000 kupitia kwa Mkuu wa Shule, Agnes Mageza ambae kulingana na utaratibu wa ukusanyaji wa fedha hizo na kuepuka matumizi yasiyo tarajiwa na fedha za maafa alilazimika kuzipeleka fedha hizo kwa Ofisa Mtendaji wa Kijiji kuhifadhiwa kwa taratibu na kutoa stakabadhi kwa kila mchangiaji kama ambavyo taratibu za upokeaji wa fedha za michago mbalimbali.
Pamoja na Waziri Pindi, Mbunge wa Jimbo la Ludewa Deo
Filikunjombe katika kuunga mkono jitihada za wapiga kura wake wakati huo alipeleka saruji mifuko 50 ili kuanza kukarabati shule hiyo huku wananchi wakichangishana kiasi cha shs milioni 1.8 kati ya zaidi ya shs milioni 13 zilizokuwa zikihitajika ili kurejesha madarasa katika hali yake na watoto wapate kusoma. Kasi ya michango kwa wananchi ilikuwa chini zaidi kwani hadi Desemba hii ni shs milioni 1.8 pekee na saruji mifuko 50 ndio iliyopatikana na kama kasi hiyo ingeendelea hivyo basi
hadi wananchi hao waweze kujenga vyumba hivyo kwa kupata shs milioni 13 basi ingekuwa ni mwakani mwezi Desemba. Kwa kuliona hilo na uchungu wa maendeleo ya elimu kwa watoto hao Mbunge Filikunjombe alilazimika kujitolea kujenga upya vyumba hivyo kwa zaidi ya shs milioni 13 ujenzi ulioanza Jumatatu wiki hii na wakati wa kujitolea kufanya hivyo Mkuu wa Shule hiyo Bi Mageza na Katibu Tarafa ya Mawengi waliwashukuru wadau mbali mbali waliochangia akiwemo Waziri Chana aliyechagia shs 15,000 ila ajabu baada ya taarifa hiyo kutoka Waziri Chana alinukuliwa akikana kuchangia maafa katika shule hiyo na hata kudai kuwa Chadema wanamchafua.
Hivyo mtandao huu wa matukio umelazimika kutafuta ushahidi
wa kile ambacho alikitoa pamoja na wengine ambao wamepata kuchangia maafa hayo kama ukweli huo unavyoonekana hapo juu. Ushauri wetu kwa Chana shule hiyo kuna majengo mengi ambayo yamechakaa hivyo si wakati wa kuanza kuruka kivuli chako mwenyewe ni wakati wa kuungana na mbunge mwenzako Filikunjombe kuleta maendeleo kwa wana Ludewa badala ya kutafuta utukufu kwa msaada usio na tija hivyo kama umeona kiasi hicho cha fedha ni fedheha jitokeze kuchangia zaidi ya ule ambao wengine wamechangia hata kujitolea milioni 20 kwa ajili ya kuboresha majengo ya shule hiyo.
Mwisho tunasema kamwe hatutakubali kuwa manabii ya uongo kukusingizia waziri Pindi Chana kwa jambo ambalo hujalifanya ili
tutaendelea kukupongeza na kukutia moyo kuzidi kuchangia kulingana na uwezo wako japo ukitoa padogo unapopongezwa usiruke kivuli chako. Wadau msikose kufuatilia sakata la waziri Pindi ambalo sasa hasira yake kaelekeza kwa waliompongeza kesho tena na siku endelea kuwa nasi matukiodaima habari bila uoga. Chanzo: www.matukiodaima.co.tz
|