Mchakato wa Usahili wa Tusker Project Fame 6 Mikoani
KAMPUNI ya Bia ya Serengeti kupitia kinywaji chake cha Tusker Lager inaendelea kuwaburudisha wateja wake mikoani na kuwapa fursa ya kushiriki usahili wa shindano la Tusker Project Fame 6 utakaofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Wananchi katika mikoa ya Arusha, Mbeya na Mwanza wananchi walipata fursa ya kuonesha vipaji vya kuimba huku wakijishindia zawadi mbalimbali zikiwemo tisheti za Tusker Project Fame, bia za bure pamoja na tiketi ya kuja Dar es Salaam katika usaili wa mashindano hayo ya kuiwakilisha Tanzania katika kinyanganyiro cha kuonesha vipaji vya kuimba Afrika Mashariki.
Washindi katika mikoa hiyo ni pamoja na David Jamal, Bartazar Kauki na Hamis S Salim na wengine wengi. Baada ya tarehe 28th – 31th 2013 kufanyika mikoa ya Arusha, Mbeya, Mwanza na Septemba Mosi shangwe hizo zilihamia jijini Dar es Salaam.
Kufuatia usahili utakaofanyika hivi karibuni wa nani ataiwakilisha Tanzania katika mashindano ya kusaka kipaji bora cha kuimba Afrika Mashariki ambao unategemewa kufanyika tarehe 7 na 8 mwezi huu, kampuni ya bia ya Serengeti imewaburudisha watanzania wa mikoni na kuwapa fursa ya kushiriki usahili huo kwa kuwapa nafasi ya kuonesha uwezo wao wa kuimba na mshindi kujipatia tiketi ya kusafiri mpaka Dar es salaam ili kushiriki katika usahili huo.
Wateja wa kampuni hiyo mkoani Arusha walijipatia tisheti, bia za bure na washindi wa kipaji cha kuimba walipata tiketi za bure za kushiriki usaili mkoani
dar es salaam. washindi hao ni pamoja na David Jamal,Bartazal Kauki na wengine wengi. pia mkoani mbeya mashindano hayo yalifanyika katika baa za Rombo Bar, Mama Land Bar na Airport Bar ambapo kila bar ilitoa mshindi na kujipatia tiketi ya kushiriki usaili.