Na Ronald Ndungi, EANA-Arusha
MCHAKATO wa shirikisho la kisiasa la Afrika Mashariki unaweza kuanza mwaka 2024, afisa mmoja wa Kenya alisema Jumatatu. Mkurugenzi Msaidizi Mwandamizi wa Masuala ya Sisa, Judy Njeri aliwaambia waandishi wa habari Nairobi, Kenya kwamba mazungumzo juu shirikisho yataanza baada ya utekelezaji kamili wa Umoja wa Fedha, inaripoti shirika huru ya habari ya Afrika Mashariki (EANA).
“Rasimu na mpango mkakati utawasilishwa kwa wakuu wa nchi za EAC Aprili,” Njeru alisema kwenye washa ya kuhamasisha waandishi wa habari.
Alisema kwamba lengo kuu la mtangamano wa EAC ni kuwa na mtangamano wenye kuwa na msingi wake toka kwa raia wenyewe wa EAC.
“Hivyo majadiliano juu ya shirikisho la kisiasa utahushisha ushiurikishwaji mpana wa mashauriano yatakayolenga kuandaa uelewa wa kufanya maamuzi na umilikaji wa mpango mzima kwa raia,” alisema.
Mkataba wa EAC unataja juu ya uanzishwaji wa shirikisho la kisiasa lakini hauelezi ni jinsi gani utaweza kupatikana. Njeru alifafanua kwamba baadhi ya vipengele ninavyoleta wasiwasi miongoni mwa nchi wanachama ni pamoja na nchi kupoteza mamlaka, tofauti za maendeleo ya kibiashara na kupotea kwa mapato ya kitaifa. Hata hivyo hatma ya uamuzi wa kuwepo kwa shirikisho la kisiasa au hapana upo mikononi mwa raia wa Afrika Mashariki kwa upigaji kura za maoni juu ya suala hiko.