Mbunge wa Kishapu kulipua bomu bungeni, ni kuhusu ubadhilifu

Mbunge imbo la Kishapu mkoani Shinyanga, Suleman Nchambi

Na Shaabani Alley, Shinyanga

MBUNGE wa Jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga, Suleman Nchambi amesema anajiandaa kutoa hoja tatu binafsi bungeni wiki ijayo kuhusu ubadhilifu wa fedha za Halmashauri ya Wilaya Kishapu.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi leo amesema kuanzia Jumatatu hii anatarajia kupeleka hoja tatu katika bunge la bajeti ikiwemo ubadhilifu wa fedha za halmashauri ya wilaya ya kishapu kiasi cha shilingi bilioni zaidi ya 6 na nusu.

Mbunge huyo amesema kuwa ataliomba bunge kutoa kauli ya kuitaka Serikali kupeleka fedha hizo ili miradi iliyosimama itekelezwe na serikali itajuana na wafanyakazi walioiba fedha hizo kwani wako katika mikono Serikali.

Alisema hoja ya pili ni maji ya mradi wa Ziwa Victoria kwa wakazi wa Shirnyanga ataliomba bunge kuitaka serikali kutambua kuwa mradi huo sio biashara kwa wakazi wa mkoa wa shinyanga kwani ni huduma na kwamba wananchi kwa sasa wanatozwa fedha nyingi kulipia maji.

Nchambi ameongeza kuwa hoja ya tatu ni Serikali kuweka sera bora za kuendeleza zao la pamba pamoja na kutangza bei mapema kwa wakulima wa zao hilo.