Mbunge Mnyika atoa shukrani na pole!

Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika

TUNAWASHUKURU sana wana Arumeru Mashariki kwa kutuongezea nguvu ya kijana Joshua Nassari. Shukrani kwa wananchi, wana-Chadema, Serikali kwa kusimamia katika ukweli wa ushindi huu wa CHADEMA! Viva CHADEMA. Hakuna kulala mpaka…Peopleeee…s….!

Poleni wananchi wa Mwanza na wapenda demokrasia na maendeleo kote nchini. Nami nimesikitishwa na naalani tukio la wabunge Highness Kiwia na Salvatory Machemli kushambuliwa kwa mapanga na mawe usiku wa kuamkia leo mara baada ya kampeni za uchaguzi wa udiwani unaofanyika leo.

Hakika tukio hili halitaishia kusikitika na kulaani, tutachukua hatua za ziada. Naendelea na mawasiliano na mashauriano na viongozi wakuu walioko Arumeru Mashariki na maeneo mengine na tutaeleza hatua zitazofuata.

Ushahidi wa kimazingira unaonyesha kwamba tukio hilo la Mwanza limefanywa na WanaCCM, ushahidi wa tuhuma za kihistoria unathibitisha kwamba CCM na serikali yake imekuwa na kawaida ya kumwaga damu nyakati za chaguzi kwa njia mbalimbali ikiwemo kwa kukata viongozi wa CHADEMA mapanga, sasa wamefikia hatua ya kushambulia viongozi wa wananchi; wabunge.

Niliwahi kutahadharisha miaka michache nyuma kwamba kadiri CCM inavyoelekea kuondoka madarakani rangi yake halisi kinyume na maneno yao ya kinafiki ya ‘kudumumisha amani na utulivu’, matendo yao halisi yatajihidhirisha ya kuwa chama na serikali inayokumbatia vitisho, vurugu na umwagaji damu kama njia ya kujaribu kujiokoa na kukataliwa na umma. Wanafanya hivyo kwa kutumia vyombo vya dola na vikosi vya chama chao vya vitisho, vurugu na umwagaji damu.

Orodha ya chaguzi ndogo za ubunge zenye matukio kama hayo ni ndefu: Kiteto (2007) wanatuhumiwa mashambulizi ya aina hiyo tena ndani ya kituo cha polisi kwa ushirikiano baina ya askari polisi na vikosi vya CCM; Tarime (2008) wanatuhumiwa kukata mapanga wanachama wa CHADEMA; Busanda na Biharamulo (2009), wanatuhumiwa kukata mapanga viongozi wa CHADEMA; Igunga (2010), walituhumiwa kummwagia tindikali mwanachama wao na kuisingiza CHADEMA na hatimaye CCM ikahusishwa na kifo cha aliyekuwa wakala wa CHADEMA Mbwana Masudi. Nyakati zote hizo Polisi walifungua majalada ya uchunguzi, watuhumiwa baadhi walitajwa kwa majina, lakini mpaka sasa hakuna aliyetiwa hatiani kwa udhalimu huo dhidi ya binadamu. Tutachukua hatua zaidi