Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema akiwa na mke wake Neema, ndani ya chumba cha mahakama kuu kanda ya Arusha jana wakati kesi dhidi yake ya kupingwa kwa matokeo ya uchaguzi ilipokuwa inasikilizwa.
MBUNGE wa Arusha Mjini kwa Tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Godbless Lema leo amefikishwa mahakamani na wakazi watatu wa Jimbo la Arusha Mjini na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mussa Mkanga, Agnes Mollel na Happy Kivuyo wakipinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu katika jimbo hilo yaliomuweka madarakani mbunge Lema.
Lema aliwasili mahakamani leo akiwa na mke wake Neema Lema, kuanza kusikiliza madai yaliyowasilishwa na wakazi hao na wanachama wa CCM kupinga matokeo yake.
wakazi watatu wa Jimbo la Arusha Mjini na wanachama wa CCM Kulia ni Mussa Mkanga,Agnes Mollel na Happy Kivuyo waliofungua kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi katika jimbo hilo kwa Mbunge wa Chadema Godbles Lema,wakiwa katika chumba cha Mkahakama Kuu Kanda ya Arusha leo wakati kesi hiyo ilipoanza kusikilizwa. (Picha zote na Janeth Mushi)