MBUNGE wa Jimbo la Kawe kupitia tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Halima Mdee ameahidi kuchangia jumla ya sh. milioni 20 ikiwa ni juhudi za mpango wa kuhakikisha kila shule ya msingi Kawe inapewa kompyuta zaidi ya mbili kwa shughuli za shule.
Halima ametoa ahadi hiyo ya fedha leo kupitia kipindi cha ‘Power Break Fast’ kinachorushwa na kituo cha redio cha Clouds FM cha jijini Dar es Salaam.
Clouds FM kupitia kipindi hicho wameanzisha mchakato wa kuchangisha fedha kwa wadau wadau anuai wanaopenda maendeleo ikiwa ni harakati za kuzisaidia shule za msingi Jimbo la Kawe kupata angalau kopyuta kwa ajili ya shughuli za shule.
Zaidi fuatilia kurasa hizi.