Mbunge Chadema Ashiriki Ujenzi Chanzo cha Maji, Tanapa Wajenga Ukumbi Olele,

Mbunge Nassar akisaidia katika hatua za awali za ujenzi wa eneo hilo.

Mbunge Nassar akisaidia katika hatua za awali za ujenzi wa eneo hilo.

 

Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki, Joshua Nassar aiwa amepanda kwenye Lori lililokuwalikibeba mawe kwa ajili ya ujenzi wa chanzo kipya cha maji
kwa ajili ya kumwagilia katika kijiji cha Karangai kata ya Kikwe katika jimbo hilo.
Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassar akishirikiana na wananchi katika kijiji cha Karangai kuweka mawe katika chanzo cha maji kwa
ajili ya umwagiliaji.
Mbunge
Joshua Nassar akizungumza na mmoja a wanakiji cha Karangai huku akiwa
amembea mtoto muda mfupi baada ya kumaliza hatua za awali za uwekaji
wa mawe kwa ajili ya ujenzi wa chanzo cha maji kwa ajili ya
umwagiliaji.
Mbunge
Joshua Nassar akizungumza na baadhi ya kina mama ambao mingoni mwao
wanajishughulisha na shughuli za kilimo alipotembelea kijiji cha
Karangai kwa ajili ya hatua za awali za ujenzi wa chanzo cha maji kwa
ajili ya umagiliaji katika kijiji hicho.
Na Dixon Busagaga
wa Globu ya Jamii kanda ya Kaskazini.

MBUNGE wa
jimbo la Arumeru Mashariki
Joshua Nassar jana ameungana na mamia ya wananchi katika kijijicha Karangai
kata ya Kikwe katika jimbo hilo kufanya shughuli za awali za ujenzi wa chanzo
kipya cha Maji kwa ajili ya umwagiliaji.
Zoezi hilo
lilo anza majira ya saa 3
asubuhi na kumalizika majira ya saa 12 jioni ilishuhudiwa Mbunge Nassar
akishiriki kazi za mikono ikiwemo kubeba mawe na kuayapanga katika eneo la mto
kwa ajili ya ujenzi wa chanzo hicho.
Akizungumza
katika eneo hilo ,Nassar
alisema lengo la ujenzi wa chanzo hicho kipya ni harakati za kuokoa mazao kwa
baadhi ya mashjamba ambayo yameanza kukauka kutokana na kukosekana kwa maji ya
kutoshja.
“Nilijitolea kulipia malori matatu kwa
siku nzima kufanya kazi hii na ununuzi wa nyaya maalum (chain link) kwa ajili
ya kufungia/kujengea Mawe kwenye eneo ambalo chanzo cha maji haya kinaanzia
lakini pia kwa sababu ilikuwa ni kazi ya kutwa nzima tulihakikisha hakuna
anayeondoka katika eneo hili hivyo tuliamua kuchinja mbuzi ,tukapika
ugali  na kazi ikaendelea”alisema
Nassar.
Nassar
aliwashukuru ijana zaidi ya 300
pamoja na kina mama waliofika katika zoezi hilo kwa lengo la kuendelea kumtia
moyo.

 

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Leonidas Gama
akisalimiana na viongozi wa wilaya ya Rombo mara baada ya kuwasili
katika shule ya sekondari Olele iliyopo kata ya Olele kwa ajili ya
kukabidhi Mradi wa ujenzi wa ukumbi wa Chakula uliojengwa kwa ufadhili
wa Shirika la Hifadhi za Taifa, Tanzania (TANAPA).

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama
pamoja na mkuu wa wilaya ya Rombo Lembris Kipuyo wakifurahia nyimbo
iliyokuwa ikiimbwa na wanafunzi wa shule ya  sekondari ya Olele
wakati alipofika kwa ajili ya uzinduizi na makabidhiano rasmi ya
ukumbi wa chakula uliojengwa kwa ufadhili wa Shirika la Hifadhi za
Taifa Tanzania (TANAPA).
RC ,Gamana iongozi wengine wakiskiliza
nyimbo iliyokuwa ikiimbwa na kwaya ya shule ya sekondari Olele
wilayani Rombo.
Kutokana na hali ya mvua iliyokuwepo wakati
wa makabidhiano ya ukumbi wa chakula,mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro
,Leonidas Gama alilazimika kubadili meza kuu na wao wakaa eneo ambalo
pia lilikuwa na mvua huku akisema ni vyema mvua ikawanyeshea wote
pamoja na wananchi.
Jengo la Ukumbi wa Chakula lililojengwa kwa
ufadhili wa Shirika la  Hifadhi za Taifa (TANAPA) katika shule ya
sekondari Olele wilayani Rombo.
Meneja Ujirani Mwema kutoka Shirika la
Hifadhi za Taifa (TANAPA) Ahmed Mbugi akitoa taarifa kuhusiana na
ujenzi wa ukumbi wa Chakula katika shule ya sekondari
Olele.
Baadhi ya wananchi katika kata ya
Olele. 
Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Hifadhi za
Taifa Tanzania,TANAPA,Ibrahim Musa akizungumza wakati wa hafla fupi ya
kukabidhi mradi wa ujirani mwema wa ujenzi wa ukumbi wa Chakula katika
shule ya sekondari Olele wilayani Rombo.
RC,Gama na DC,Kipuyo wakilowa kutokana na
mvua iliyokuwa ikiendelea kunyesha.
Wanafunzi katika shule ya sekondari Olele
wakifuatilia hotuba ya viongozi waliofika shuleni hapo kwa ajili ya
makabidhiano ya ukumbi wa chakula uliojengwa na
TANAPA.
Mkuu wa wilaya ya Rombo ,Lembris Kipuyo
akizungumza katika hafla hiyo.
Wakazi wa kata ya Olele.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama
akihutubia wananchi waliofika katika hafla fupi ya makabidhiano ya
ukumbi wa chakula uliojengwa katika shule ya sekondari Olele wilayani
Rombo kwa ufadhili wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania
(TANAPA)
Mkuu wa mkoa wa Kilimajaro ,Leonidas Gama
akikagua jengo hilo.