Mbowe, Lisu chupu chupu kukamatwa!

Mwenyekiti wa Chama Cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe.

Na Mwandishi Wetu, Arusha

MWENDESHA Mashitaka wa Serikali Wakili Haruni Matagane, katika kesi
inayomkabili Mwenyekiti na Katibu wa Chama Cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki na wafuasi wao 25 jana ameiomba mahakama kutoa hati ya kukamatwa kwa Mwenyekiti na Mbunge huyo kwa kile kutofika mahakamani.

Hata hivyo Mahakama ilipuuza ombi Matagane baada ya wakili wa utetezi, Method Kimomogolo Mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Devotha Msofe, kuwatetea wateja wake kuwa walishindwa kufika kwenye kesi hiyo baada ya kubadilika kwa ratiba ya ndege waliopanga kuja nayo.

Awali Matagane aliieleza mahakama hiyo kutokufika kwa watuhumiwa hao ni ukiukwaji wa sheria za Mahakama hivyo kushauri wakamatwe, kauli ambayo haikuweza kuzaa matunda.

Akiwatetea mahakamani wateja wake wakili wa upande wa utetezi, Kimomogolo aliieleza mahakama hiyo kuwa Freeman Mbowe na Tindu Lisu wameshindwa kufika mahakamani baada ya ndege waliyokuwa wasafiri nayo kubadilisha ratiba.

Kimomogolo alidai kuwa watuhumiwa hao walikuwa katika kikao juzi hadi
usiku ila jana walitarajia kuja mjini hapa kwa ndege ila imeshindikana kutokana na ndege hiyo kuahirisha safari.

“Jamhuri bado inasisitiza arrest warranty kwa Lissu na Mbowe zitolewe
na mahakama kwani walikwua wanajua shauri hili linakuja leo mahakamani kama ni vikao vingefanyika walau siku mbili kabla ya kesi,” alisema Matagane

Wakili wa utetezi alilazimika kusimama tena mahakamani hapo na kudai
kuwa, washitakiwa hao wameshindwa kufika mahakamani kutokana na ndege
kuahirisha safari hivyo kama wakili wa Serikali anawahitaji
waje, shauri hilo liahirishwe kwa muda ili kuwasubiri mpaka
watakapofika.

“Kesi inakuja kwa ajili ya kutajwa tunaamini kuwa hiyo wamechelewa kwa sababu ndege imeahirishwa kama ni busara tupange tarehe nyingine ya kesi kutajwa.” alisema Kimomogolo.

“Hii ni mahakama haiwezi kumsubiri mshtakiwa kama wakili wao angeleta
vielelezo kuhusiana na suala hili ili mahakama iweze kuamini madai yao ya kushindwa kufika, Mheshimwia msimamo wetu ni arrest warrant kwani hawajatii amari ya kufika mahakamani leo,” alisema Wakili Matagane

Kwa upande wake hakimu Msofe alikubaliana na sababu ya Wakili wa
upande wa utetezi na kusema kuwa haoni sababu ya kutoa hati ya
kukamatwa kwa washitakiwa hao. Msofe alidai kuwa Hakimu anayesikiliza shauri hilo (Devotha Kamuzora) angekuwepo ndiye angeweza kuzingatia maombi hayo ya kutoa hati ya kukamatwa, kwani yeye yupo kwa ajili ya kuahirisha shauri hilo. Wakili wa serikali aliiomba mahakama hiyo kupanga tarehe ya kuanza usikilizwaji wa awali wa kesi hiyo kwa madai kuwa upelelezi wa shauri hilo umekamilika.

Naye wakili wa utetezi Kimomogolo,aliieleza mahakama hiyo kuwa
kutokana na mahakama kipindi cha mwisho wa mwaka kuwa katika mapumziko ya mwaka kesi hiyo ipangwe siku ya kutajwa na Hakimu Kamuzora apange siku ya kuanza kuisikiliza kesi hiyo. Hakimu huyo aliahirisha shauri hilo Disemba 20 mwaka huu ambapo litatajwa na kupangiwa siku ya kuanza usikilizwaji wa awali.

Kosa la kwanza linalaowakabili washitakiwa wote 27 ni kufanya
kusanyiko kinyume cha sheria na kutokutii amri ya polisi Peter Mvula,
kuwa shitaka la pili likiwa ni kutotii amri halali ya polisi
iliyotolewa na Mvula ya kuwataka kutawanyika katika viwanja vya NMC
ya kuwataka watawanyike.

Alidai kuwa Novemba 7 mwaka huu majira ya usiku hadi novemba 8 saa 12
asubuhi katika viwanja hivyo walishiriki kusanyiko haramu, huku shitaka la tatu linamkabili Slaa peke yake ambapo anadaiwa kutoa maneno ya uchochezi katika mkutano huo.

Aidha kesi hiyo namba 454 ya mwaka 2010, ni baada ya viongozi hao
kufanya mkesha katika viwanja vya NMC Unga Limited mjini hapa kushinikiza kuachiwa kwa Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema(CHADEMA) aliyekuwa gereza la Kisongo vaada ya kukataa dhamana katika kesi ya kufanya maandamano na mkutano usio halali, akitokea mahakaamni baada ya kuhudhuria kesi inayomkabili ya kupingwa kwa matokeo yake ya uchaguzi.