Mbio za Mwenge kuzindua miradi ya bil. 1.7 Arusha

Mwenge wa Uhuru pichani.

Na Janeth Mushi, Arusha

MIRADI 11 ya Maendeleo yenye thamani ya zaidi ya sh. bilioni 1.7 ambayo imegharamiwa na Serikali Kuu, kwa kushirikiana na halmashauri, wahisani pamoja na wananchi inatarajiwa kuzinduliwa katika mbio za mwenge wa Uhuru.

Aidha mwenge huo uliowashwa Kijijini Butiama mkoani Mara jana kwa lengo la kumuenzi Baba wa taifa Hayati Nyerere ambapo utazimwa Disemba 9 mwaka huu siku ya kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika.

Kwa mujibu wa taaarifa iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo kwa vyombo vya habari jana, inasema kuwa mwenge huyo uatwasili mkoani hapa octoba 16 mwaka huu wilayani Ngorongoro katika eneo la “Nabi Gate”.

Taarifa hiyo pia inasema kuwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge mwaka huu ambaye ni Mtumwa Khalfan na mwenge huo utakimbizwa mkoani hapa kwa siku mbili ambapo utakimbizwa katika wilaya za Ngorongoro, Monduli na Arusha Mjini.

Aidha mkesha huo wa wmenge utakwua katika eneo la Mto wa Mbu wilayani Monduli Oktoba 16, Oktoba 17 utakuwa wilayani Arusha Mjini katika eneo la Soko la Mbauda na Oktoba 18 utakabidhiwa mkoani Kilimajaro. Kauli mbiu ya mwenge kwa mwaka huu ni kusheherekea miaka 50 ya uhuru ambayo ni “Tumethubutu, tumeweza na tutazidi kusonga mbele.”

Mkuu huyo wa mkoa alitoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Arusha hususani wale ambao maeneo yao yatatembelewa na mwenge wa uhuru, kujitokeza kwa wingi ili kuweza kusikiliza ujumbe wa kiongozi huyo wa mbio za mwenge kitaifa. Hayati Baba wa Taifa Nyerere alifariki dunia Oktoba 14 mwaka 1999 Hospitali ya Mtakatifu Thomas huko Uingereza, ambapo madaktari walisema alikuwa akisumbuliwa na kansa ya damu (leukemia).