Mazishi ya siri ya Gaddafi

Kanali Muammar Gaddafi

MAMLAKA nchini Libya zinafanya mipango ya kufanya mazishi ya siri kwa kiongozi aliyeondolewa madarakani Kanali Muammar Gaddafi, baada ya kukamatwa na kuawa, BBC inafahamu.
Hata hivyo, inaonekana huenda kukawa na kuchelewa kufayika kwa mazishi hayo, ambayo chini ya utamaduni wa Kiislam mazishi hufanyika haraka iwezekanavyo.
Waziri wa mafuta Ali Tarhouni ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa mwili wa Kanali Gaddafi huenda ukahifhadhiwa “kwa siku kadhaa”.
Nato inatarajiwa ktangaza kumalisha shughuli zake nchini Libywa katika saa chache zijazo.
Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy amesema kifo cha Gaddafi kinamaanisha shughuli za kijeshi za Nato nchini Libwa zimefikia mwisho wake.
“Ni wazi shughuli hiyo imefikia kikomo,” amewaambia waandishi wa habari.
Mapema, waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Alain Juppe alisema shughuli za Nato zitamalizika “baada ya kuzingatia hatua kadhaa za mpito katika wiki moja ijayo”.

-BBC