Mazishi ya Padri Evaristus Mushi Zanzibar

Vijana waumini wa Dini ya Kikiristo wakiteremsha jeneza lenye mwili wa marehemu Padri Evaristus Gabriel Mushi, katika kaburi alilozikwa katika viwanja vya kanisa la Katoliki la Kitope, Wilaya ya Kaskazini B Unguja, marehemu alifariki kwa kupigwa risasi Jumapili iliyopita na watu wasiojulikanwa.[Picha na Ramadhan Othman, IKULU]

Misa ya kumuombea marehemu Padri Evaristus Gabriel Mushi kutoka Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akiwasalimia wananchi wakati alipofika katika Kanisa la Minaramiwili Mjini Zanzibar kutoa salamu ya Mwisho
kwa Padri Evarist Gabriel Mushi aliyefariki kwa kupigwa risasi na watu wasijuilikanwa Jumapili iliyopita na amezikwa Kijini Kitope Wilaya ya Kaskazini B Unguja.[Picha na Ramadhan Othman Ikulu]

Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Zanzibar Augustino Shao, akitia udongo katika kaburi la Marehemu Padri Evaristus Gabriel Mushi, aliyezikwa leo katika viwanja vya kanisa Katoliki la Kitope, Wilaya ya Kaskazini B Unguja.[Picha na Ramadhan Othman, IKULU]

ASkofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam Muadham Policup Kadinari Pengo,kwa pamoja na maaskofu wengine wakichomeka Msalaba katika kaburi la marehemu Padri Evaristus Gabriel Mushi,aliyezikwa katika viwanja vya kanisa Katoliki la Kitope, Wilaya ya Kaskazini B Unguja,ambae alifariki Jumapili Iliyopita kwa kupigwa risasi na watu wasiojukanwa.[Picha na Ramadhan Othman,IKULU]

Baadhi ya waumini wa kanisa katoliki wakiwa katika mazishi ya marehemu Padri Evaristus Gabriel Mushi,aliyezikwa katika viwanja vya kanisa Katoliki la Kitope,Wilaya ya Kaskazini B Unguja, ambae alifariki Jumapili Iliyopita kwa kupigwa risasi na watu wasiojukanwa.[Picha na Ramadhan Othman, IKULU]

Rais wa Zanbzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt,Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Zanzibar Augustino Shao, wakielekea katika Mazishi ya Padri Evaristus Gabriel Mushi aliyezikwa katika viwanja vya kanisa la Kitope, Wilaya ya Kaskazini B Unguja.[Picha na Ramadhan Othman, IKULU]