
Baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki wa Marehemu Mzee Constantine Munishi Kyara wakitoa heshima za mwisho kwenye ibada ya mazishi iliyofanyika mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro.

Padre wa Kanisa Katoliki Parokia ya Moshi Mjini, akiongoza ibada ya mazishi ya Marehemu Mzee Constantine Munishi Kyara iliyofanyika eneo la Rau, nje kidogo ya mji wa Moshi, Kilimanjaro juzi.

Mke wa Marehemu Mzee Constantine Munishi Kyara, (wa pili kulia waliokaa) akifarijiwa na baadhi ya wajukuu zake, wengine ni ndugu jamaa na marafiki zake wakimfariji.

Mke wa Marehemu Mzee Constantine Munishi Kyara, (katikati) akiwa kwenye mbada ya mazishi ya mumewe juzi.

Mtoto wa marehemu mzee Constantine Munishi Kyara, Oscar Munishi (wa kwanza kushoto) ambaye pia ni mfanyakazi wa kampuni ya Simu ya Airtel Tanzania jinini Dar es Salaam wakiwa na mkewe kwenye ibada ya mazishi juzi.

Baadhi ya wajukuu wa marehemu Mzee Constantine Munishi Kyara, wakibeba jeneza la babu yao kuelekea kaburini.

Baadhi ya wajukuu wa marehemu Mzee Constantine Munishi Kyara, wakisaidiana na baadhi ya waombolezaji kushusha mwili wa babu yao kaburini.

Mke wa Marehemu Mzee Constantine Munishi Kyara, (aliyeshika taji) akiweka taji hilo kwenye kaburi la mumewe juzi

Mke wa Marehemu Mzee Constantine Munishi Kyara, (aliyeshika taji) akiweka taji hilo kwenye kaburi la mumewe huku akisaidiwa.