
Mtoto mkubwa wa kike wa marehemu Mary Magaya Magaya, Catherine Paschal akisaidiwa na waombolezaji baada ya kuishiwa nguvu kwa majonzi alipokuwa akitoa heshima za mwisho katika mwili wa mamayake.

Baadhi ya watoto wa kiume na ndugu wa karibu wa marehemu Mary Magaya wakiwa katika ibada ya kumuombea marehemu kwenye Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya waombolezaji wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Mary Magaya katika Kanisa Katoliki la Mt. Joseph Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam.

Baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu Mary Magaya wakiingia kwenye magari tayari kwa msafara wa kuelekea makaburini mara baada ya ibada ya kumuombea marehemu.

Baadhi ya ndugu wa karibu na waombolezaji wakiwafariji watoto wa kike wa marehemu Mary Magaya eneo la makaburi ya Tandika wakati shughuli za mazishi zikiendelea.