MaxMalipo Wazinduwa Huduma Mpya kwa Simu ya Kiganjani

Mkuu wa kitengo cha Biashara Maxcom Africa Bw. Deogratius Lazari (Katikati) Akifafanua Jambo kwa waandishi wa habari ambao hawapo katika picha wakati wa Uzinduzi wa Mfumo Mpya wa kutoa huduma za Maxmalipo kwa kutumia simu ya kiganjani, wengine katika picha ni  Maasifisa wa Kampuni Kulia msimamizi mauzo na Usambazaji kanda ya mashariki Bwan Bw. Thomas Mwakalembile na Geofrey Mwakamyanda

Mkuu wa kitengo cha Biashara Maxcom Africa Bw. Deogratius Lazari (Katikati)
Akifafanua Jambo kwa waandishi wa habari ambao hawapo katika picha wakati wa
Uzinduzi wa Mfumo Mpya wa kutoa huduma za Maxmalipo kwa kutumia simu ya
kiganjani, wengine katika picha ni Maasifisa wa Kampuni Kulia msimamizi mauzo na Usambazaji kanda ya mashariki Bwan Bw. Thomas Mwakalembile na Geofrey Mwakamyanda

 
MAXCOM Maxcom Africa maarufu kama MaxMalipo ni kampuni ya kitanzania iliyoanzishwa mwaka 2010
ambayo imewekeza katika kurahisisha maisha ya Watanzania na Waafrika kwa ujumla
kiuchumi na kijamii kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya mawasiliano (ICT
Technology).
 
Ili kufikia malengo na Sera ya Taifa ya kutumia mifumo ya kielekroniki kutoa huduma
na pia kuwezesha Watanzania walio wengi kufikiwa na huduma hizi (Financial
Inclusion)  na pia  kurahisisha ukusanyaji wa kodi na kuongeza
ajira, MaxMalipo imeanzisha huduma  mpya
itakayomuwezesha mtanzania kulipa bili zote kwa kutumia simu ya kiganjani  aina ya
Smart phone yenye Mfumo utakaojulikana kama SmartMalipo.
 
Huduma hii inatarajiwa kutoa ajira kwa watanzania takribani laki mbili (200,000)  nchi nzima kufikia mwaka 2016  na hivyo kuchangia ukuaji wa sekta isiyo rasmi
ya ajira na kunyanyua uchumi wa Nchi. 

Mfumo huu utaweza kurahisisha ulipaji wa bili mbalimbali Mfano; Umeme
(Luku), Ving’amuzi vya Televisheni, Vocha za Mitandao yote, Kulipia Kodi za TRA
na Baadae Kufanya Miamala ya Kibenki  inayohusisha Kuweka na Kutoa fedha, huduma
ambazo kwa sasa zinalipwa kupitia mashine za MaxMalipo.
 
Huduma hiyo inapatikana kwenye mfumo wa simu ya kiganjani ambapo mtumiaji atalazimika
kuweka  mfumo wa SmartMalipo (Download
Smart Wakala Application) kutoka tovuti ya Google play au tovuti ya Maxmalipo
kwa  kuandika neno ‘SmartMalipo  au Maxmalipo’.
Kisha mtumiaji atapata maelekezo ya  jinsi ya ku-install mfumo huu
kwenye simu yake na jinsi ya kutumia. Mfumo huu utamwezesha mtumiaji yeyote kuwa
Wakala na kulipia huduma zilizo orodheshwa. 
Mtumiaji
 wa  mfumo huu  atajipatia kamisheni kama alivyo wakala
mwingine wa Maxmalipo kwa Huduma atakazofanya.
 
 
Watumiaji wa mfumo huu wa SmartMalipo watatambulika kwa jina la ‘Smart Wakala’ popote
walipo na kufanya biashara kupitia simu zao za kiganjani. 
MaxMalipo
imeanzisha huduma hii mpya kwa lengo la kuwawezesha watanzania walio wengi
kufikiwa zaidi na
  huduma za malipo kwa haraka wakiwemo wafanyabiashara wadogo na wenye mitaji midogo  ambao kwa mazingira yao ni vigumu kuwa na
Mashine za Maxmalipo.
 
 
 MaxMalipo imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza matatizo ya foleni kwenye malipo ya huduma mbalimbali kama bili za TRA, LUKU, DAWASCO, huduma za kibenki na hata katika mifuko ya Hifadhi ya jamii Mfano PSPF.