Mawaziri wa Fedha Nchi za Ukanda wa Afrika Wajadili Maendeleo
Na Ingiahedi Mduma, Abidjan
MAWAZIRI wa Fedha wa Nchi za Ukanda wa Afrika wamekutana mjini Abidjan kwa lengo la kujadili masuala anuai ya maendeleo kwa nchi zao.
Akizungumza na vyombo vya habari mchana huu DK. Likwelile ambaye amemuwakilisha Waziri wa Fedha na katika Mkutano wa Benki ya Dunia amesema kuwa; “Mkurungezi wa Kanda ametoa ripoti ya mwaka, ameelezea ni namna gani ukanda huu wa Afrika ulivyokuwa ukifanya kazi za maendeleo, ameelezea ripoti hiyo kuwa inagusa nchi zote sita za Afrika. Nchi hizo ni pamoja na Rwanda, Tanzania,Uganda, Kenya, Ethiophia na Visiwa vya Shelisheli, Aidha nchi hizo zimefanya kazi vizuri.
Likwelile amefanafua kuwa, “Mkurugenzi wa ukanda wanchi za Afrika ameelezea jinsi uchumi unavyokua kwa kasi kubwa kwani umekua kwa asilimia sita mpaka saba na ukuaji huu wa uchumi unawanufaisha watu wote wa nchi hizo.
Ni Muhimu kuwekeza kwenye reli hii itawapunguzia wananchi usumbufu wanaoupata kwenye masuala ya usafiri na usafirishaji wa mizigo.Aliongeza Likwelile.
Pia Likwelile amezungumzia kuhusu kuendeleza kilimo hasa kilimo chenye tija. alisema kuwa kilimo cha biashara humuongezea kipato mwananchi wa chini na kumfanya kujikwamua kwenye hali ya kimasikini.
Aidha mwenyikiti amezungumzia suala nishati hasa nishati ya umeme ili tuweze kuendelea ni muhimu kusimamia suala la umeme kwa kikanda. Hii itapelekea nchi zote za Afrika kunufaika na masuala ya maendeleo kiujumla kwa nchi hizo za kikanda.
“Mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi mkuu wa rais, Aidha ukanda wa nchi za Afrika unapenda kumshukuru raisi aliyepita Dk. Kaberuka kwa kazi nzuri aliyoifanya kwani ameziacha nchi katika hali nzuri sana” Alisisitiza Likwelile
Mwisho Likwelile alifafanua kuwa, “Benki ya Maendeleo ya Afrika imetambua umuhimu wa kazi na mchango mkubwa alioutoa Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete na ndio maana imemualika katika Mkutano huu wa mwaka kutokana na kazi zuri aliyoifanya.