Mauaji Wakenya; Mkuu wa Polisi Kenya Ajiuzulu

Inspekta Generali Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Kenya, David Kimaiyo.

Inspekta Generali Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Kenya, David Kimaiyo.

INSPEKTA Generali Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Kenya, David Kimaiyo ametangaza kujiuzulu ikiwa ni shinikizo kutokana na yeye kushindwa kuwajibika juu ya matukio kaadhaa ya ushambulizi toka kwa wanamgambo wa kundi la Al Shabaab yanayoendelea kupoteza maisha ya raia wa Kenya.

Generali Kimaiyo ametangaza uamuzi huo huku yeye akiuita kustaafu mapema kutokana na kushindwa kuwalinda raia wa nchi hiyo, hali iliyopelekea kufanyika kwa mashabulio kadhaa yaliyogharimu maisha ya Wakenya. Hivi karibuni Kenya imeshambuliwa na wahalifu waliojitaja kuwa wanamgambo wa Al Shabaab katika mashambulizi mawili ambalo moja lilipoteza maisha ya rais 26 kabla ya shambulio lingine la juzi lililouwa Wakenya 36.

Wakati huo huo Rais Uhuru Kenyatta amemteuwa Waziri Mkuu mpya wa usalama, Joseph Nkaiseri kuchukua nafasi ya aliyekuwa Waziri wa Usalama, Joseph Ole Lenku. Rais Kenyatta alisema kuwa baada ya mazungumzo na Kimaiyo alikubali ombi lake la kustaafu mapema majukumu yake ili kuwapisha wengine kufanya kazi hiyo.

Kundi la wanamgambo nchini Somalia Al Shabaab limekiri kuwaua watu 36 katika shambulio lililotokea kwenye machimbo ya kokoto karibu na mji wa Mandera kaskazini mwa Kenya. Katika taarifa iliyotolewa kwenye mtandao wa kundi hilo, wanamgambo hao wamesisitiza kuwa ndio waliowaua wakenya hao kwa sababu ya majeshi ya Kenya kuendelea kuwa nchini Somalia.

Taarifa za mauaji hayo zilitolewa kwa mara ya kwanza na Shirika la Msalaba Mwekundu. Inaarifiwa kuwa wafanyakazi hao walipigwa risasi wakiwa katika mahema ya. Walioshuhudia shambulizi walisema kwamba wapiganaji hao waliwatenga waisilamu na wakristo huku wakiwachinja baadhi, na kuwapiga risasi wlaiosalia.

Wakazi wa eneo hilo wamesema waathirika wote wa tukio hilo ni watu wasio Waislam ambao walikuwa wakifanya kazi katika machimbo hayo yaliyopo Kormey kilomita 15 kutoka mji wa Mandera Kaskazini mwa Kenya. Tukio hili linafuatia tukio la wiki moja iliyopita ambapo watu wapatao 28 waliuawa katika shambulio la basi la abiria huko Mandera.

-BBC