Matukio ya JK Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Mashujaa
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiamkiana na wazee wa Tanzania Legion waliopigana katika vitra kuu ya dunia ya pili waliohudhuria kwenye Maadhimisho ya siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa yaliyofanyika katika bustani ya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam Julai 25, 2014. PICHA NA IKULU.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Mohamed Ali Shein kwenye Maadhimisho ya siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa yaliyofanyika katika bustani ya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam. Wengine ni Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Ghalib Bilali na Waziri Mkuu Mzengo Pinda Julai 25, 2014.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwela ngao kwenye mnara wakati wa Maadhimisho ya siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa yaliyofanyika katika bustani ya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam Julai 25, 2014.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa kasimama kikakamavu wakati wimbo wa Taifa ukipigwa kwenye Maadhimisho ya siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa yaliyofanyika katika bustani ya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam Julai 25, 2014.