MATUKIO YA AWALI YA KUAPISHWA KWA BARAZA LA MAWAZIRI IKULU

Waziri wa Maji Mh. Marck Mwandosya akiingia katika viwanja vya Ikulu akiwa na Familia yake tayari kwa kula kiapo.

Waziri wa Mambo ya Nje Mh. Bernald Membe katika picha muda mfupi kabla ya kuapishwa katika viwanja vya Ikulu ambapo mawaziri na manaibu waziri katika wizara mbalimbali wataapishwa na Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete

Mh. Bernald Membe waziri wa Mambo ya Nje kushoto akisalimiana na Waziri wa Ulinzi Mh. Hussein Mwinyi.

Mustafa Mkulo Waziri wa Fedha kushoto akipongezana na Waziri wa Ulinzi Mh Hussein Mwinyi.Msemaji wa Wizara ya Fedha Ingiahedi Mduma akisalimiana na mdau Anna Itenda wa Idara ya Habari Maelezo.