Prof. Laura Fair, aliyefanya utafiti na kutunga kitabu cha wa mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad, akizindua kitabu hicho wakati wa uzinduzi wa Taasisi ya mwanaharakati huyo iliofanya jana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shei,(hayupopichani) katika ukumbi wa Salama Hall Bwawani Hotel mjini Unguja,ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi, alipohudhuria katika Uzinduzi wa Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad, katika ukumbi wa Salama Hall Bwawani Hotel ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za miaka 50 ya mapinduzi Ya zanzibar (katikati) Bibi Nasra Mohamed Halal Mwenyekiti wa Taasisi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (katikati) Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi, (kushoto) akiwa mlezi wa Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad akifuatiwa na Mwenyekiti wake Bibi Nasra Mohamed Halal, wengine kulia Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Said Ali Mbarouk, wakiwa katika Uzinduzi wa Taasisi hiyo iliyozinduliwa katika ukumbi wa Salama Hall Bwawani Hote, ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar. [Picha zote na Ramadhan Othman, Ikulu.]