Meneja Uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi, akiwakaribisha wageni waalikwa kwenye hafla ya uzinduzi wa shindano la Big Brother HOTSHOTS msimu wa tisa iliyoandaliwa maalum kwa wadau wa DStv na waandishi wa habari usiku wa kuamkia leo kwenye hoteli ya Dar es Salaam Serena.
Bi. Kambogi alitoa rai kwa Watanzania kuwa wazalendo kwa kuwapigia kura nyingi washiriki wetu wawili wanaoiwakilisha nchi kwenye shindano hilo na kutoa angalizo kwa wazazi na walezi kuhusiana na shindano hilo wanaotakiwa kuangalia ni wenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea, ili kudhibiti watoto wasiangalie wanaweza kufanya hivyo kupitia rimoti zao kuwa kuweka namba za siri kwenye chaneli hiyo.
Na Mwandishi wetu
Shindano linalopendwa na wengi barani Afrika, maarufu la Big Brother Afrika ambalo kwa mwaka huu ni la msimu wa 9 likijulikana kama Big Brother Hotshot lililoanza usiku wa kuamkia leo Tanzania imeng’ara hasa kwa washiriki wake kufanya vizuri katika muonekano wa awali sambamba na shoo iliyopigwa na mwanamuziki Nasseb Abdul ‘Diamond’ aliyeteka umati uliohudhuria uzinduzi huo.
Halfa hiyo ya masaa mawili ambayo imeweza kushuhudia washiriki 26, imekuwa gumzo pale washiriki wanaoiwakilisha Tanzania msimu huu wa 9, Laveda na Idriss wakifanya kweli katika utambulisho wao huku mwanamuziki Diamond akikonga vilivyo na wimbo wake wa ‘My Number One’.
Tanzania imekuwa na bahati ya kipekee kwa mshiriki wake huyo, Laveda ambapo aliteka umati mkubwa kwa kuonesha uhodari wake wa kupuliza “Saxophone”, hali iliyopelekea kupigiwa kura nyingi huku akishangiliwa kwa shangwe muda wote.
Kura hizo alizopigiwa Laveda na kuwa juu ya washiriki wote 26, pia zimemfanya awe Mkuu wa jumba hilo ‘Head of the House’ mpaka hapo itakapoamuliwa na Biggy. Kura alizopigiwa Laveda ni 85.0 huku mshiriki wa Kenya, Sabina akipata kura 78.3, ambaye yeye alionyesha uwezo wake wa kuchekesha kwa kutumia maneno.
Kwa upande wa mshiriki mwingine wa Tanzania, Idriss naye aliweza kukonga nyoyo za wageni wa jumba hilo waliofurika kwenye uzinduzi ambapo yeye aliweza kucheza kwa ustadi wimbo maalum. Uchezaji wake na mavazi aliyoyavaa yaliweza kuwa kivutio kikubwa huku akishangiliwa muda wote, ambapo aliweza kupigiwa kura na kupata alama zaidi ya 60.
Mpaka hatua ya mwisho, muongozaji wa BBA, IK alieleza kuwa, Tanzania imekuwa kinara kwa washiriki wake hao hasa baada ya kuonyesha kipaji cha hali ya juu.
Meneja Uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi, alitoa rai kwa watanzania kuwapigia kura washiriki hao iliweze kufika mbali hata kunyakua taji la shindano hilo.
Barbara aliwataka watanzania kuendelea kufuatilia shindano hilo, huku wakipata wasaha wa kupiga kura kwa njia mbalimbali ikiwemo kwa mitandano ya kijamii, simu ya mkononi na nyinginezo.
Shindano hilo la kila mwaka, linaloandaliwa na kampuni ya Multchoice, linashirikisha washiriki kutoka nchi 14 za bara la Afrika na mshindi anatarajiwa kuondoka na kitita cha dola 300,000.
Baadhi ya nchi hizo zilizotoa washiriki ni pamoja na Angola, Botswana, Afrika Kusini, Tanzania, Uganda, Kenya, Malawi, Zambia, Namibia, Ghana, Nigeria, na Zimbabwe.
Shindano hilo lililoanza rasmi 2003, Tanzania imekuwa ikifanya vizuri kwa washiriki wake, akiwemo Mwisho Mwampamba pamoja na Richard Bezuidenhout ambao waliweza kung’ara ikiwemo Richard aliyewahi kutwaa taji hilo.
Bi. Emelda Mwamanga Mtunga na Shamim Mwasha wakipata ukodak.
Tanzania shangwe zatawala
Kwa upande wa Tanzania, shangwe zilitawala kwa wadau mbalimbali waliokuwa wakishuhudia uzinduzi huo moja kwa moja kwenye halfa maalum iliyoandaliwa na DStv Tanzania ndani ya hoteli ya Serena, ambapo walipongeza huku wakiahidi kuwapa sapoti kubwa washiriki wao.
Baadhi ya wadau hao wakiwemo watu maarufu walioungana na wandishi wa habari, team ya DStv Tanzania na wateja wa DStv akiwemo Aliyekuwa Mwakilishi wa Tanzania katika Shindano la msimu wa 7 wa Big Brother Stargame 2012 Julio Batalia.
Walisema washiriki hao wameonyesa mwanzo mzuri hivyo kila mtanzania anatakiwa kujivunia na hata kuwapa sapoti.
Mwandishi wa gazeti la The African, Sidi Mgumia (katikati) akipata ukodak na wadau.
Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Mauzo wa Hoteli ya DoubleTree by Hilton Dar es Salaam, Florenso Kirambata, Blogger Seif Kabelele, Blogger Jestina George Meru #Diaspora na Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania, Bi. Furaha Samalu.
Wageni waalikwa wakipata Ukodak.
Wageni waalikwa wakinywa na kubadilishana mawazo wakati wa sherehe za uzinduzi wa Big Brother HOTSHOTS uliofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye hoteli ya Serena Dar es Salaam.
Bloggers wakipata ukodak na Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania, Bi. Furaha Samalu (wa pili kushoto).
Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania, Bi. Furaha Samalu akibadilishana mawazo na Aliyekuwa Mwakilishi wa Tanzania katika Shindano la msimu wa 7 wa Big Brother Stargame 2012 Julio Batalia (kulia) wakati wa sherehe za uzinduzi wa shindano la Big Brother HOTSHOTS lilizinduliwa usiku wa kuamkia leo na kuwapa fursa wadau wa DStv na waandishi wa habari kushuhudia Live kwenye big screen kubwa ndani ya hoteli ya Dar es Salaam Serena.
Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania, Bi. Furaha Samalu akipata ukodak na mshiriki huyo.
Baadhi ya wageni waalikwa wakipozi kupata ukodak.
Meneja Uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi akipata ukodak na Blogger Shamim Mwasha wa 8020 Fashions.
Meneja Uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi, akishow love na msanii wa muziki nchini aliyewahi kutumbuiza kwenye moja ya shindano la Big Brother Africa C.P ak.a CPWAA.
Blogger Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog akibadilishana mawazo na Mike Mushi wa Jamii Forums (kushoto) kwenye hafla hiyo iliyofana ndani ya hoteli ya Dar es Salaam Serena usiku wa kuamkia leo.
Meneja Uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi akibadilishana mawazo na Mbunifu wa mavazi wa kimataifa nchini, Sheria Ngowi wakati hafla ya uzinduzi ikiendelea.
Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania, Bi. Furaha Samalu (katikati) akipata ukodak na Mike Mushi wa Jamii Forum na Blogger Seif Kabelele.
Mkurugenzi wa Mauzo wa Hoteli ya DoubleTree by Hilton Dar es Salaam, Florenso Kirambata akipata ukodak na warembo Christina Sintah pamoja na Jacqueline Mzindakaya (kushoto). (Picha zote na Zainul Mzige wa MOblog).