Kikundi cha Brass Band cha Umoja wa Vijana CCM Zanzibar, kikiongoza matembezi ya maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar, yaliyofunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, kuanzia Micheweni kuelekea Wete Mkoa wa Kasakazini Pemba.
Vijana wa CCM Zanzibar, UVCCM wakiwa katika Matembezi ya maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yaliyofunguliwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, (hayupo pichani)yaliyoanzia Micheweni kuelekea Wete Mkoa wa Kasakazini Pemba. [Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, alipokuwa akizungumza na Umoja wa Vijana wa CCM Zanzibar na Wanachama wa CCM Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba pamoja na kuyafungua Matembezi ya Umoja huo ya Maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar, katika uwanja wa Mpira Micheweni kwa Shaamemata, (kushoto) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, akipokea risala ya UVCCM Zanzibar baada ya kusomwa na naibu katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Zanzibar Shaka Hamdu Shaka, katika ufunguzi wa Matembezi ya Umoja huo, ya kuadhimisha Miaka 50 ya Mapinduzi, katika uwanja wa Mpira Micheweni kwa Shaamemata, Mkoa wa kaskazini Pemba.
Vijana wa Chama cha Mapinduzi, UVCCM wa Mikoa na Wilaya wakiwa katika uwanja wa Mpira wa Micheweni kwa Shaamemata, Mkoa wa Kaskazini Pemba, wakisubiri ufunguzi wa matembezi ya umoja huo ya kuadhimisha Miaka 50 ya Mapinduzi na kufunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar.
Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Sadifa Juma Khamis akizungumza na Wanachama wa CCM na Wananchi wakati alipokuwa akimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, kuzungumza na Umoja wa Vijana ili kuyafungua Matembezi ya Maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar, katika uwanja wa Mpira Micheweni kwa Shaamemata, Mkoa wa Kaskazini Pemba,[Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar akisalimiana na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Sadifa Juma Khamis, alipowasili katika uwanja wa Mpira Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba, katika ufunguzi wa matembezi Umoja wa Vijana wa CCM Zanzibar katika kuadhimisha miaka 5o ya Mapinduzi. [Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]