
Mgeni rasmi na Mwanaharakati kutoka nchini Uganda, Bi. Miriam Mutembe akiwasili katika viwanja vya TGNP Mabibo jijini Dar es Salaam. Walioongozana naye ni Bi. Usu Mallya Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP (kushoto) na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya TGNP, Ruth Meena.
Mgeni rasmi na Mwanaharakati kutoka nchini Uganda, Bi. Miriam Mutembe akisalimia waalikwa wengine wa tamasha la jinsia.

Mgeni rasmi na Mwanaharakati kutoka nchini Uganda, Miriam Mutembe akitoa mada leo katika
Tamasha la Jinsia Tanzania 2013 .

Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania, Deus Kibamba akiwasilisha mada yake kwa wanaharakati waliohudhuria tamasha la jinsia.

Waandishi kutoka katika mikoa mbalimbali ambao pia ni wanaharakati kutoka mikoa anuai wakiwa katika picha ya pamoja kwenye viwanja vya TGNP, Mabibo.
Baadhi ya wanatamasha pamoja na wageni anuai wakifuatilia mada na burudani zinazotolewa katika uwanja wa tamasha hilo.