Gwaride la Sherehe za Miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Amani Mjini Zanzibar leo kwa ajili ya kuhudhuria katka sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar. Picha na OMR
Msanii Halikuniki akiongoza Kikundi cha wasanii cha Cha Beni Maarufu(Mbwakachoka) kikipita mbele ya mgeni
rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi DK. Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani) katika sherehe za kutimia miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, zilizofanyika leo katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Zanzibar [Picha na Ramadhan Othman, Ikulu]
Wafanyakazi wa Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar wakipita mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi DK. Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani) katika sherehe za kutimia miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, zilizofanyika leo katika Uwanja
wa Amaan Studium Mjini Zanzibar.[Picha na Ramadhan Othman, Ikulu]
Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda, Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama mwanamwema Shein, na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Davis Mwamunyange, wakiwa katika Jukwa la VIP katika kilele cha Sherehe za Miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar [Picha na Ramadhan Othman, Ikulu]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduizi Dk.Ali Mohamed Shein,akitoa hutuba yake kwa wananchi wa Zanzibar kupitia katika sherehe za kutimia miaka 49 ya Mapunduzi Matukufu ya Zanzibar huko Uwanja wa Amaan Studiuma Mjini Zanzibar jana, kuhudhuriwa na Maelfu ya wananchi mbali mbali Mjini na Mashamba.[Picha na Ramadhan Othman, Ikulu]
Kikosi cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kikipita mbale ya Rais kwa Gwaride la Mwendo wa kuruka ruka, katika sherehe za Kutimia miaka 49 ya Mapinduzi Matiukufu ya Zanzibar huko
Uwanja wa Amaan Studium Mjini Zanzibar jana. [Picha na Ramadhan Othman, Ikulu]
Kikosi cha Jeshi la (KMKM) Kikosi cha kuzuia Magendo Wanaume kikipita mbale ya Rais kwa Gwaride la Mwendo wa haraka, katika sherehe za Kutimia miaka 49 ya Mapinduzi Matiukufu ya Zanzibar huko Uwanja wa Amaan Studium Mjini Zanzibar jana. [Picha na Ramadhan Othman, Ikulu]