Waziri wa Fedha Saada Salum Mkuya akiwa pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa CITI na Mkuu wa Afrika kwa kundi la sekta ya utumishiwa umma Bw. Peter M. Sullivan alipo mtembelea Waziri kwa madhumuni ya kuisadia nchi ya Tanzania katika ubalozi wa Marekani mjini Washington DC.
Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya alipokutana na Makamu wa Rais JICA anayesimamia nchi za Afrika, Bw. Kato Hiroshi na Bw. Kiyoshi Kodera ambaye ni Makamu wa Rais kiongozi katika Benki ya Dunia, walipokuja kuelezea nia yao ya kutaka kuendelea kuleta miradi nchini Tanzania. Maongezi hayo yalifanyika katika ukumbi wa ubalozi wa Marekani mjini Washington DC.
Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya wa katikati akiwa pamoja na ujumbe kutoka Tanzania walipokutana na Mkurugenzi msaidizi na Mkuu wa idara ya Afrika sehemu ya Mashariki Bw. Herve’ Joly walipokuwa wakijadiliana na kuangalia ni jinsi gani Tanzania imeweza kutekeleza sera za Shirika la fedha la Kimataifa mjini Washington DC.
Waziri wa Fedha Saada Salum Mkuya akimsikiliza kwa makini Bi. Diana Layfield ambaye ni Mtendaji mkuu wa kanda ya Afrika, alipokuwa akieleza mambo ambayo Standard Chartered inaweza kuyafanya katika kuendeleza uchumi wa Tanzania mjini Washington DC
Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile walipokuwa na Naibu katinu Mkuu Marekani Bw. W.L. Mc Donald nje ya jengo la Hazina Marekani.