Mjane wa Hayati Nelson Mandela, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Graca Michel Trust (GMT), Bi. Graca Michel (kulia) akishangilia baada ya kutuma ujumbe mfupi kwa njia ya simu za viganjani kwa simu zote zilizosajiliwa nchini Tanzania ikiwa ni ishara ya uzinduzi kampeni za kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike zitakazoendeshwa mkoani Mara.
Baadhi ya wanafunzi wakiangalia ujumbe mfupi uliotumwa kwa simu zote zilizosajiliwa kwa njia ya simu za kiganjani na Mjane wa Hayati Nelson Mandela, Bi. Graca Michel kwa kushirikiana na Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Bi. Sophia Simba kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike.
Baadhi ya viongozi wa mashirika mbalimbali walioshiriki hafla ya uzinduzi wa kampeni za kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike zitakazoendeshwa mkoani Mara. Uzinduzi huo umefanywa na mjane wa hayati Nelson Mandela, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Graca Michel Trust, Bi. Graca Michel leo jijini Dar es Salaam.
Viongozi mbalimbali wastaafu wa Serikali, viongozi wa dini Mkoa wa Mara, wawakilishi wa wanafunzi Mkoa wa Mara wakiwa katika hafla ya uzinduzi rasmi wa kampeni za kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike zitakazoendeshwa mkoani Mara.
Mjane wa Hayati Nelson Mandela, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Graca Michel Trust (GMT), Bi. Graca Michel akisalimiana na baadhi ya viongozi mbalimbali kutoka mkoani Mara.
Mjane wa Hayati Nelson Mandela na Mwenyekiti wa Taasisi ya Graca Michel Trust (GMT), Bi. Graca Michel akimbusu mmoja ya watoto wa kike kutoka Mkoa wa Mara kuonesha ishara ya upendo katika uzinduzi huo.
Mjane wa Hayati Nelson Mandela, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Graca Michel Trust (GMT), Bi. Graca Michel (kulia) akizungumza kabla ya kuzindua rasmi kampeni za kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike zitakazoendeshwa mkoani Mara.
Baadhi ya wanafunzi wakitumbuiza katika hafla ya uzinduzi rasmi wa kampeni za kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike.
Baadhi ya washiriki katika hafla ya uzinduzi rasmi wa kampeni za kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike zitakazoendeshwa mkoani Mara. Uzinduzi huo umefanywa na mjane wa hayati Nelson Mandela, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Graca Michel Trust, Bi. Graca Michel leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Valerie Nsoka akizungumza katika hafla hiyo.
Igizo katika hafla hiyo.
Hafla ya Uzinduzi Kampeni Kupinga Ndoa Utotoni Dar ikiendelea.
Rais mstaafu Benjamin William Mkapa akisalimia washiriki katika hafla hiyo.
Baadhi ya viongozi wa mashirika mbalimbali walioshiriki hafla ya uzinduzi wa kampeni za kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike zitakazoendeshwa mkoani Mara. Uzinduzi huo umefanywa na mjane wa hayati Nelson Mandela, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Graca Michel Trust, Bi. Graca Michel leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanahabari…!