Kapteni Emmanuel Kukula (aliyenyoosha kidole) wa Jeshi la Wananchi Tanzania akiwa na baadhi ya maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa pamoja na Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu wakishauriana masuala ya Protokali kabla ya kuanza kwa sherehe za maadhimisho ya miaka 69 ya Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa kwake zilizofanyika leo jijini Dar es Salaam kwenye viwanja vya Karimjee.
Na Mwandishi wetu
WASHIRIKA wa maendeleo wametakiwa kutimiza ahadi yao ya kuwezeshwa kuanzishwa kwa mfuko wa mabadiliko ya hali ya hewa (GCF) kwa kuchangia dola za Marekani bilioni 100 kila mwaka hadi kufikia mwaka 2020.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ardhi , Nyumba na maendeleo ya makazi Profesa Anna Tibaijuka wakati wa sherehe za Umoja wa Mataifa kufikisha miaka 69 katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam.
Aidha alisema ni muhimu pia watekeleze ahadi ya fedha, uhamishaji wa teknolojia na uwezeshaji ili mataifa yanayoendelea yaweze kuhakikisha kwamba yanabadili mifumo yao ili kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Katika sherehe hizo zilizofanywa kwa shamrashamra kubwa pamoja na gwaride, Profesa Tibaijuka alisema juhudi hizo zinazoelekezwa na Umoja wa Mataifa hazina budi kufuata kanuni za Rio ambapo kuna nia moja ya kukabili mabadiliko ya hali ya hewa na wajibu tofauti.
Aidha alisema pamoja na Tanzania kutekeleza wajibu wake inaamini kwamba viongozi wa wadunia wakiwa mstari wa mbele katika mkutano ujao wa Lima ambao unaandaa mkutano wa Paris mwakani watawezesha makubaliano bora yanayotekelezeka.
Brigadia Jenerali Dominc Basil Mrope wa JWTZ (kushoto) akiwasili kwenye viwanja vya Karimjee na kuelekea jukwaa kuu.
Pamoja na kuzungumzia uwajibikaji katika masuala ya kukabili mabadiliko ya tabia nchi Waziri Tibaijuka alizungumzia mafanikio ya Tanzania katika kutekeleza malengo ya milennia na kusema kwamba yale yaliyobaki yataendelea kufanyiwa kazi ili kusukuma mbele zaidi maendeleo.
Alisema serikali kwa sasa imelenga kuendeleza yale ambayo hayajakamilika kwa kutengeneza mpango wa maendeleo unaoana na malengo ya milennia yaliyobaki.
Awali akimkaribisha Waziri, Mratibu mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa shirika la maendeleo la UNDP, Alvaro Rodriguez, alisema yapo mambo ambayo bado yanalegalega katika utekelezaji wa malengo ya milennia na Umoja wa Mataifa utaendelea kuisaidia Tanzania kuyakamilisha.
Alisema pamoja na Tanzania kupiga hatua kubwa katika masuala ya elimu ya msingi, usawa wa jinsia, vifo vya watoto, uzuiaji wa maambukizi ya Ukimwi na kufanikisha upatikanaji wa maji safi na salama bado kuna changamoto kubwa katika kukabiliana na umaskini na vifo vya wanawake katika uzazi.
Balozi wa Sweden nchini Tanzania Mh. Lennarth Hjelmaker akiwasili kwenye viwanja vya Karimjee na kupokelewa na afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na kuelekea jukwaa kuu.
Rodriguez amesema kwamba mashirika ya Umoja wa Mataifa kwa sasa yanasaidia katika kukabiliana na upungufu katika maeneo husika huku wakisubiri majadiliano na serikali kuhusu mipango ya maendeleo baada ya kupita kwa muda wa mwisho wa malengo ya milenia.
Aidha amesema kwamba kwa sasa kuna program 10 zinazofanywa na mashirika ya Umoja wa Mataifa kuimarisha demokrasia ya Tanzania na haki za binadamu, makabiliano na Ukimwi vifo vya akina mama wakati wa uzazi na uimarishaji wa ajira kwa vijana.
Akitaja mafanikio ya mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Mratibu huyo alisema kwamba asilimia 96 ya zahanati na vituo vya afya nchini Zanzibar vimewezesha hudma za mama na mtoto na karibu kila kituo kina tabibu mmoja anayeshughulikia masuala hayo.
Aidha mfumo wa haki za mtoto umeimarishwa na wakimbizi wapatao 60,000 Nyarugusu wamepatiwa haki za msingi kama maji na elimu.
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushi (katikati) akibadilishana mawazo na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kulia) pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajabu Gamaha(kushoto) kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 69 ya Umoja wa Mataifa zilizofanyika leo kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar.
Mkuu wa uendeshaji na ushauri wa Ofisi za Umoja wa Mataifa Tanazania Bw.George Otoo akibadilishana mawazo na Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) hapa nchini Bw. Damien Thuriaux kabla ya kuanza rasmi kwa sherehe hizo.
Mgeni rasmi Waziri wa Ardhi , Nyumba na maendeleo ya makazi, Profesa Anna Tibaijuka akiwasili kwenye viwanja vya Karimjee huku akiwa ameongozana Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.
Baadhi ya wakuu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania wakiwa wamejipanga tayari kumlaki mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya miaka 69 ya Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa kwake Profesa Tibaijuka. Kulia ni Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akihakikisha Protokali zimezingatiwa.
Pichani juu na chini ni Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akimtambulisha mgeni rasmi Waziri wa Ardhi , Nyumba na maendeleo ya makazi Profesa Anna Tibaijuka kwa baadhi ya wakuu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini mara baada ya kuwasili kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 69 ya Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa kwake.
Waziri wa Ardhi , Nyumba na maendeleo ya makazi, Profesa Anna Tibaijuka akipokea heshima ya wimbo wa taifa kabla ya kuanza rasmi kwa sherehe za maadhimisho miaka 69 ya Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa kwake.
Waziri wa Ardhi , Nyumba na maendeleo ya makazi, Profesa Anna Tibaijuka akikagua gwaride maalum kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 69 ya Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa kwake zilizofanyika leo jijini Dar.
Waziri wa Ardhi , Nyumba na maendeleo ya makazi, Profesa Anna Tibaijuka akishuhudia bendera ya Umoja wa Mataifa ikipandishwa kama ishara ya kuadhimisha miaka 69 ya Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa kwake.
Mshehereshaji wa sherehe za maadhimisho ya miaka 69 ya Umoja wa Mataifa Maulida Hassan kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akitoa mwongo wa hotuba mbalimbali kwa meza kuu.
Mgeni rasmi Waziri wa Ardhi , Nyumba na maendeleo ya makazi, Profesa Anna Tibaijuka akisoma risala kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 69 ya Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa kwake yaliyofanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar.
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akisoma ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 69 ya Umoja wa Mataifa zilizofanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar.
Waziri wa Ardhi , Nyumba na maendeleo ya makazi, Profesa Anna Tibaijuka akipongeza Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez kwa hotuba nzuri.
Makamu Mwenyekiti wa Asasi ya Umoja Mataifa (UNA), Bw. Benedict Kikove akizungumza kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 69 ya Umoja wa Mataifa yaliyofanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar. (Picha zote na Zainul Mzige)