Matukio ndani ya viwanja vya Saba Saba leo

 

Msimamizi wa Huduma kwa Wateja wa kampuni ya Simu ya Tigo, Boaz Ikupilika akionesha medemu maalumu ya internet ikiwa ni moja ya huduma zinazotolewa na kampuni hiyo ndani ya banda lao viwanja vya SabaSaba jana.

 

Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Mahusiano wa EWURA, Titus Kaguo alipokuwa akizungumza na wanahabari kutoa ufafanuzi juu ya mabadiliko ya tozo ya bei ya kodi ya mafuta ya taa.

 

Hapa ndipo tulipo ZANTEL ndani ya viwanja vya Sabasaba. "Zantel High Life" karibu.

Hapa sio Beach, bali ni ndani ya Banda la Zantel huduma ya High Life ndani ya viwanja vya SabaSaba. Tembelea ujionee mwenyewe.

Delphin Bernrd Kallghe, akionesha moja ya samani za vyuma zinazotengenezwa na kampuni yake ya MR OIL SKUVI 141 LIMITED

 

Hapa ndipo lilipo Banda la Airtel ndani ya viwanja vya Sabasaba; "Hamia Airtel". Baadhi ya wahudumu wa kampuni ya Airtel wakipata maelekezo ya namna ya kutoa huduma zao kwa wateja ndani ya Sabasaba jana

Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Simu za Mkononi Airtel wakielekezana jambo ndani ya Banda lao Sabasaba jana.