
Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicholas Musonye (kushoto) akifungua Kliniki ya wanahabari kuripoti habari za Mashindano ya Kombe la Tusker Chalenji jana.

Meneja wa Bia ya Tusker, Rita Mchaki (kushoto) kutoka kampuni ya Bia ya Serengeti Breweries (SBL) akihudhuria Kliniki hiyo, Bi. Mchaki alikuwa ni mmoja wa wazungumzaji katika hafla hiyo ya wanahabari.

Baadhi ya wanahabari kutoka nje ya nchi waliohudhuria Kliniki hiyo

Sehemu ya wanahabari waliopata mafunzo hayo ya kuripoti habari za Mashindano ya Kombe la Tusker Chalenji.

Baada ya Kliniki ilifuata mechi kati ya timu ya Wanahabari wa Tusker Chalenji Tanzania dhidi ya Timu ya Wanahabari wa Tusker Chalenji kutoka nchi za nje, mchezo uliofanyika katika viwanja vya Leader jijini Dar es Salaam. Wanahabari wa Tanzania walishinda 3-0.

Hiki ni kikosi cha Wanahabari wa Mashindano ya Kombe la Tusker Chalenji wakiwa katika picha ya pamoja. Mchezo huu kati ya wanahabari wa Tanzania na wale wa nje ya Tanzania ulimalizika kwa Watanzania kushinda 3-0.