Matukio Mazishi Msiba wa Bi. Kudude Zanzibar

Vijana waliobeba Jeneza la mwili wa Marehemu Msanii maarufu Fatma Binti Baraka (kidude) wakati wa maziko yake yaliyofanyika leo huko kijijini kwao Kitumba, Wilaya ya Katri Unguja,ambapo maziko yake yamehudhuriwa na wasanii mbali mbali ndani na nje ya nchi. [Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,(wa nneĀ  kulia) akijumuika na viongozi na waislamu katika kumswalia Marehemu Msanii maarufu Fatma Binti Baraka (kidude)
katika msikiti wa Mwembeshauri Mjini Unguja leo.[Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,(kutoka kulia) Rais wa jamhuri ya Muungano Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, Makamo wa Kwanza wa Rais Zanzibar Maalim Seif
Sharif, na Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi, wakiitikia dua baada ya maziko ya Msanii maarufu Fatma Binti Baraka (kidude) aliyefariki jana na kuzikwa leo Kijijini kwao Kitumba, Wilaya ya Katri Unguja. [Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]

Baadhi ya Wananchi waliohudhuria katika maziko ya marehemu Bi Fatma Baraka (Kidude) kijijini kwao Kitumba, Wilaya ya Katri Unguja. [Picha na Ramadhan Othman Ikulu]


Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ,Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo kwenye kaburi la Msanii mkongwe wa Muziki wa Mwambao (Taarab) Tanzania,Marehemu Fatma Baraka (Bi Kidude) katika makaburi ya Kitumba Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.