Kaimu Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia Tanzani TGNP, Lilian Liundi (katikati), akitoa hotuba yake wakati wa kongamano la wazi la jamii kujadili mchakato wa kutengeneza katiba mpya. (kushoto), Mdau wa Maendeleo Humphrey Polepole, na kulia Mwanaharakati wa Masuala ya Kijamii na Haki za Binaadamu, Gemma Akimali.
Kushoto, Kaimu Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia Tanzani TGNP, Lilian Liundi akiteta jambo na Mwanaharakati wa Masuala ya Kijamii na Haki za Binaadamu, Gemma Akimali.
Mwanaharakati na aliyekuwa Mjumbe wa Kamati iliyokusanya maoni ya wananchi katika mchakato wa katiba mpya, Humphrey Polepole akichangia mada katika kongamano hilo.
Baadhi ya wanaharakati pamoja na wana jamii wakiwa kwenye Kongamano la kujadili mchakato wa kutengeneza katiba mpya kwenye viwanja vya TGNP, Mabibo Dar es Salaam.

Mambo muhimu yaliojadiliwa katika kongamano hilo ni pamoja na ilani ya wanawake katika katiba mpya kuangalia suala la usawa wa kijinsia, wanawake wanapataje haki zao za msingi hasa katika suala la matibabu, uzazi salama, elimu, maji salama, ushiriki wa kutosha katika nafasi za ajira ngazi zote. Mengine ni pamoja na ushiriki sawa katika nafasi za maamuzi na ulinzi wa kutosha kutokana na kukithiri kwa ukatili wa Kijinsia. Kongamano hilo lilifanyika Agosti 6,2014 kwenye viwanja vya TGNP jijini Dar es Salaam. Picha zote na Philemon Solomon.