Matukio katika ziara ya mtandao wa dev.kisakuzi.com kuangalia huduma za msingi kwa watu wenye ulemavu na uenezwaji wa taarifa juu ya Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Walemavu wilayani Arumeru kwa ufadhili wa ICD

Kikundi cha Wanapambazuko Klabu cha Shule ya Msingi Iliboru wilayani Arumeru, kikiwa katika picha ya pamoja. Kikundi hichi hufanya hamasa na kuelimisha jamii juu ya haki anuai za watoto wenye ulemavu eneo hilo ikiwa ni juhudi za ICD.

Bi. Vick Kimaro ambaye ni mmoja wa viongozi wawakilishi wa watu wenye ulemavu wilayani Arumeru, akionesha nakala ya chapisho lililoandaliwa na Kituo cha Habari Kuhusu Ulemavu linalounadi Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Watu wenye Ulemavu alipozungumza na mwandishi wa mtandao huu (hayupo pichani).

Mwalimu Mkuu wa Kituo cha Wanafunzi wenye Ulemavu, Shule ya Msingi Naurei wilayani Arumeru, Tuzie Mtenga akizungumza na mtandao wa dev.kisakuzi.com kufafanua shughuli anuai za kituo hicho juzi

*Ziara ya mtandao wa dev.kisakuzi.com mkoani Arusha kuangalia huduma za msingi kwa watu wenye ulemavu wilayani Arumeru kwa ufadhili wa Kituo cha Habari Kuhusu Ulemavu (ICD)

Mwalimu Mratibu wa Kituo cha Walemavu cha Shule ya Msingi Iliboru, Loitusho Yamat akifafanua jambo kwenye mahojiano na mtandao wa dev.kisakuzi.com jana wilayani Arumeru

Baadhi ya wanafunzi wa darasa la nne (viziwi) katika Kituo cha Walemavu cha Shule ya Msingi Iliboru wakiandika darasani

Mwanafunzi Richard Kisanga (18) wa Kituo cha Walemavu cha Shule ya Msingi Naurei ya wilayani Arumeru akinakili hesabu kama alivyopewa maelekezo na mwalimu wake

Baadhi ya walimu waliopo katika mafunzo ya vitendo katika Kituo cha Walemavu cha Shule ya Msingi Iliboru wakifundisha darasa la saba

Mmoja wa wanafunzi wenye ulemavu (kiziwi), Shule ya Msingi Iliboru akiandika darasani kama alivyokutwa na mpiga picha wa Thehabari.com