Matukio Katika Picha Ziara ya dev.kisakuzi.com Namanyere, Nkasi

Huku kwetu Kata ya Kirando, wilayani Nkasi Bucha kuandikwa hivi sio tatizo, kwa kuwa tunakubaliana na kuvumiliana...! Pichani ni moja ya bucha linalochinja nyama kwaajili ya wakristu.

Huku kwetu Kata ya Kirando, wilayani Nkasi Bucha kuandikwa hivi sio tatizo, kwa kuwa tunakubaliana na kuvumiliana…! Pichani ni moja ya bucha linalochinja nyama kwaajili ya wakristu.

Uhamasishaji utamaduni wa kunawa mikono kwa afya, pichani ni eneo maalumu la kuosha mikono mara baada ya shughuli anuai zinazo iacha mikono si salama kiusafi. Hapa ni Katika moja ya Shule za Sekondari Kirando.

Na hii ndiyo shule ya sekondari iliyobuni utaratibu huo wa kuosha mikono.

Na hii ndiyo shule ya sekondari iliyobuni utaratibu huo wa kuosha mikono.

Maboti
IMG_0338

Pichani juu ni baadhi ya maboti yanayotumika kusafairisha abiria kutoka Kata ya Kirando, Nkasi kwenda vijiji vya jirani Ziwa Tanganyika

Pichani juu ni baadhi ya maboti yanayotumika kusafairisha abiria kutoka Kata ya Kirando, Nkasi kwenda vijiji vya jirani Ziwa Tanganyika

Usione udogo wa boti hili maalumu kwa kubeba mizigo lina uwezo wa kubeba gunia 1000 za bidhaa anuai...!

Usione udogo wa boti hili maalumu kwa kubeba mizigo lina uwezo wa kubeba gunia 1000 za bidhaa anuai…!

Mwandishi wa mtandao wa dev.kisakuzi.com, Joachim Mushi (kulia) akizungumza na mmoja wa wadau wa usafirishaji abiria alipokuwa katika ziara ya kutembelea vijiji kadhaa vya Wilaya ya Nkasi, Rukwa.

Mwandishi wa mtandao wa dev.kisakuzi.com, Joachim Mushi (kulia) akizungumza na mmoja wa wadau wa usafirishaji abiria alipokuwa katika ziara ya kutembelea vijiji kadhaa vya Wilaya ya Nkasi, Rukwa.

Huku tunalima kwa kutumia mifugo kama huyu. Pichani ng'ombe wakitoka kutimiza wajibu wao (kulima).

Huku tunalima kwa kutumia mifugo kama huyu. Pichani ng’ombe wakitoka kutimiza wajibu wao (kulima).

Mwandishi wa dev.kisakuzi.com akiangalia kimea cha mahindi ambacho hutumika kutengenezea pombe aina ya komoni moja ya vijiji vya Nkasi.

Mwandishi wa dev.kisakuzi.com akiangalia kimea cha mahindi ambacho hutumika kutengenezea pombe aina ya komoni moja ya vijiji vya Nkasi.

Huku ni mbali kutoka mjini lakini Serikali imetukumbuka na tunalo 'gari' la wagonjwa. Moja ya pikipiki zinazotumika kama gari la wagonjwa kituo cha afya Kirando.

Huku ni mbali kutoka mjini lakini Serikali imetukumbuka na tunalo ‘gari’ la wagonjwa. Moja ya pikipiki zinazotumika kama gari la wagonjwa kituo cha afya Kirando.

Baada ya kazi sasa ni wakati wa ugali na mkebuka..! Asante ziwa Tanganyika, waujua mkebuka wewe..!

Baada ya kazi sasa ni wakati wa ugali na mkebuka..! Asante ziwa Tanganyika, waujua mkebuka wewe..!