Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake katika picha ya pamoja na viongozi wa Taasisi ya Elimu ya Ufundi ya Singapore baada ya kutembelea kampasi yao jijini Singapore Juni 6, 2013.
Baadhi ya wafanyabiashara walioongozana na Rais Jakaya Kikwete katika ziara ya kikazi nchini Singapore wakiwa katika picha ya kumbukumbu na mawaziri walio katika msafara huo Juni 6, 2013. . Wa pili kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe akifuatiwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Dk Abdallah Kigoda na Waziri wa Uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe (wa tatu) kulia.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake wakitembezwa kwenye makao makuu ya Mamlaka ya Ustawishaji Upya wa Miji Upya ya Singapore Juni 6, 2013 ambapo wanajionea mfano wa jiji hilo ukiwa umetengenezwa mahususi kwa kuhakikisha mji unapangwa na kusimamiwa kisayansi kwa mipango miji ya muda mfupi na muda mrefu.
Mojawapo ya vivutio vikubwa katika jiji la Singapore ni hoteli hii ya kitalii na casino iitwayo Marina Bay ambayo kuna jengo la mgahawa lenye umbo la meli juu ya majengo yake mawili
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake wakitembelea Taasisi ya Elimu ya ufundi (Institute of Technical education) iliyo sawa na VETA kwa Tanzania Juni 6, 2013. ambapo pamoja na mambo mengine walijionea jinsi wanafunzi wake wanavyofundishwa kuunda vipuli vya aina mbalimbali ikiwa ni pamoja na vya ndege
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake katika picha ya pamoja na viongozi wa Mamlaka ya Ustawishaji Upya ya Miji ya Singapore Juni 6, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake wakitembezwa kwenye makao makuu ya Mamlaka ya Ustawishaji mijini ya Singapore Juni 6, 2013.ambapo wanajionea mfano wa jiji hilo ukiwa umetengenezwa mahususi kwa kuhakikisha mji unapangwa na kusimamiwa kisayansi kwa mipango miji ya muda mfupi na muda mrefu