Matukio Katika Picha Sherehe za Mei Mosi Mkoani Kilimanjaro

Mtafiti kutoka kituo cha utafiti wa zao la Kahawa ncini cha TACri ,Jeremiah Magesa akitoa maelezo mbele ya mgeni rasmi namna ambayo  kituo  hicho kinavyo saidia katika upatikanaji wa mbegu bora ya zao la Kahawa.

Mtafiti kutoka kituo
cha utafiti wa zao la Kahawa ncini cha TACri ,Jeremiah Magesa akitoa
maelezo mbele ya mgeni rasmi namna ambayo kituo hicho
kinavyo saidia katika upatikanaji wa mbegu bora ya zao la
Kahawa.

Wafanyakazi wa
Shirika la Umeme(TANESCO) mkoa wa Kilimanjaro wakipita na gari lao
mbele ya mgeni rasmi katika sherehe za Mei Mosi zilizofanyika katika
uwanja wa Chuo Kikuu chaUshirika  mjini
Moshi. 
Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) wakipita katika maonesho ya Mei
Mosi Mkoani Kilimanjaro.
Chuo cha wauguzi
Kibosho pia walipita mbele ya mgeni rasmi kuonesha nini wanafanya
katika sherehe hizo za Meio Mosi.
Moja ya mtambo inayotumika kunyunyiza dawa katika Kahawa ikioneshwa mbele ya mgeni rasmi.
Kampuni ya Swissport
pia walikuwepo kuonesha kazi wanayofanya katika viwanja vya
ndege.
Kassim Mwinyi akitoa
maelezo kuhusu kampuni ya Panone inavyosaidia katika utoaji wa huduma
ya mafuta.
Mwakilishi wa
kampuni ya Bia Tanzania ,Pudensiana akitoa maelezo kuhusu kampuni
hiyo.
Magari ya kampuni ya
TBL yakipita mbele ya mgeni rasmi.
Baaadhi ya wa
wafanyakazi wakifuatilia maonesho hayo.
Afisa Masoko wa
Hifadhi ya taifa ya mlima Kilimanjaro (KINAPA)Antypas Mgungusi akitoa
maelezo juu ya ofa iliyotolewa na hifadhi hiyo ya kupanda mlima
Kilimanjaro hadi kilele cha Shira kwa gharama za Kiasi cha sh
25.000ikijumuisha kiingilio hifadhini,usafiri wa kwenda na kurudi ofa
inayotaraji kuanza rasmi Mei 15 mwaka huu.
Halmashauri ya
manispaa ya Moshi wakionesha shughuli mbalimbali wanazofanya pamoja na
kikombe cha mshindi wa pili wa usafi.
Mstahiki Meya wa
Manispaa ya Moshi ,Jafary Michael akikabidhi kikombe cha ushindi wa
nafasi ya pili katika usafi pamoja na cheti kwa mgeni rasmi kaimu mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro,Novatus Makunga katika shrehe za Meio mosi
zilizofanyika katika uwanja wa chuo kikuu cha
Ushirika.
Bodi ya Kahawa
Tanzania TCB pia walikuwepo katika sherehe hizo.
Watengenezaji wa
Highlife Gin pia waipita kutangaza bidhaa zao mele ya mgeni
rasmi.
Kampuni ya SBC
watengenezaji wa kinywaji cha Pepsi na jamii yake pia walipita
kuonesha vinywaji vinavyo tengenezwa nakampuni hiyo.
Kampuni ya Sukari ya
TPC ilitia fora baada ya kuingiza mitambo yake inayotumika katika
kilimo,kunyunyiza dawa pamoja na kupakia miwa wakati wa
uvunaji.
hata hivyo vijana
walikosa uvumilivu wakalazimka kukimbilia miwa iliyoachwa uwanjani
hapo kwa ajili ya maonesho.
Wafanyakazi wakiimba
wimbo wa Solidarity katika shrehe hizo.
Na Dixon Busagaga wa
Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.