Matukio Katika Picha Bungeni Leo Mjini Dodoma

Naibu Spika, Dk. Tulia Akson akizungmza na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiku baada ya kusitisha Bunge kwa ajili ya mapumziko mchana wa leo.

Naibu Spika, Dk. Tulia Akson akizungmza na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiku baada ya kusitisha Bunge kwa ajili ya mapumziko mchana wa leo.

 

 

 

Wabunge wakijadiliana jambo walipokuwa wakiingia bungeni Dodoma.

 

 

 

 

 

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Rukwa, Bupe Mwakang’ata (kulia), akijadiliana jambo na Mbunge wa Viti Maalumu, Joyce Sokombi kwenye viwanja vya Bunge, Dodoma

Naibu Waziri wa Afya, Dk. Hamisi Kigangwalah akijibu maswali ya wabunge

Mbunge wa Viti Maalumu, Mkoa wa Iringa, Ritta Kabati (kushoto) akiwa na Mbunge wa Viti Maalumu, Oliva.

 

Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akizungumza na Mbunge  wa Newala Vijijini, George Mkuchika.

Wanafunzi wa Shule ya ADC NARCO ya wailayani Kongwa wakiwa bungeni Dododma kuona mwenendo wa bunge hilo.

 

Spika wa Bunge, Job Ndugai akiwasihi wabunge kuwa na tabia ya kuheshimiana baada ya Mbunge wa Mbozi, Haonga kumwambia yeye amekula maharage gani kiasi kwamba hawaoni kuwapa nafasi ya kuchangia hoja wabunge wanaokaa nyuma.

 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Watu Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama, akitangaza bungeni, Dodoma, kutengua baadhi ya kanuni ili mwili wa aliyekuwa Spika wa Bunge, marehemu Samuel Sitta uingie bungeni leo kwa ajili ya kuagwa na wabunge. Kulia ni Mwansheria Mkuu wa Serikali, George Masaju.

 

 

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Mashariki, Kolimba (kushoto) na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makaz, Anjelina Mabula wakiingia bungeni