Matukio Katika Maadhimisho ya Miaka 67 ya Wiki ya Umoja wa Mataifa Tanzania

Mwakilishi mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Alberic Kacou akitoa salaam za Umoja wa mataifa wakati wa maadhimisho ya 67 ya Umoja huo leo jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samuel Sitta akizungumza na wageni mbalimbali waliohudhuria sherehe za maadhimisho ya 67 ya wiki ya Umoja wa Mataifa katika viwanja vya Karimjee leo jijini Dar es Salaam. Pamoja na mambo mengine amesisitiza juu ya umuhimu wa nchi za bara la Afrika kutathmini na kupima mafanikio ya malengo 8 ya millennia pamoja na kuongeza juhudi katika kupambana na umasikini na janga la njaa.


Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samuel Sitta akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kupokea maelezo ya awali kutoka kwa Ofisa Habari na Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Hoyce Temu (kulia) kuhusu mabanda ya maonyesho yaliyoandaliwa rasmi kuonyesha shughuli mbalimbali zinazofanywa na umoja wa mataifa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali nchini Tanzania.


Wanafunzi wa shule ya sekondari Azania wakiimba wimbo uliobeba historia na mafanikio ya Umoja wa mataifa tangu kuanzishwa kwake leo jijini Dar es salaam wakati wa maadhimisho ya 67 ya wiki ya Umoja wa Mataifa.(Picha zote na Aron Msigwa – MAELEZO)